Mh. Kessy kaiambia VOA TV News kuwa kata yake ya Kaloleni ndiyo kata pekee ambayo inaongoza kwa usafi katika jiji la Arusha ukizingatia kata hiyo ipo katikati ya jiji la Arusha.
Aidha Diwani huyo amewataka wakazi wa kata hiyo kuwa wasafi kwa kutotupa takataka hovyo hovyo na endapo mtu yoyote atabainika kutupa takataka hovyo atapigwa faini ya Tsh. 50,000.
'Mzee wa Nukta' amekuwa akishiriki kikamilifu katika kushughulika na masuala yahusuyo jamii moja kwa moja huku wananchi wakimuunga mkono kwa jitihada zake.
Katika hatua nyingine Diwani Huyo pia Amewapongeza Lions Club Arusha kwa jitihada zao za kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma ya Afya jicho bure kwa wakazi wa jiji la Arusha.
Zoezi hili lilifanyika hapo Jana katika Makumbusho ya azimio la Arusha ambapo Lions Club walitoa misaada mbalimbali ya Vipimo, Dawa, Miwani na maji kwa watu waliofika eneo hilo kupima macho. Shughuli ambayo ilifanywa sambamba na Hospitali ya Mkoa Mount Meru na (H) jiji la Arusha.
0 Comments:
Post a Comment