HABARI: Golugwa aitwa TAKUKURU

Taarifa iliyotolewa October 18, mwaka huu na ofisi za chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zimesema Katibu Wa Kanda ya kaskazini na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa ameitwa kwenye ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini,  (TAKUKURU) huku ikiwa haijulikani sababu za wito huko.


Golugwa anaitwa na TAKUKURU   ikiwa ni siku baada ya taasisi hiyo kumuonya  Mbunge wa Arumeru Mashariki  Joshua Nasari kuwa asiishinikize  Taasisi kufanya kile anachotaka badala yakawaache wafanyie kazi ushahidi aliowasilisha juu ya namna   madiwani wa CHADEMA walivyorubuniwa kwa rushwa na kukihama chama hicho..

"Katibu wa Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha #Mhe.Amani Golugwa amewasili leo TAKUKURU saa 3 kamili asubuhi.

Mhe.Katibu alipokea wito akiitajika kufika katika Ofisi za TAKUKURU Arusha siku ya leo Oktoba 18."

0 Comments:

Post a Comment