Askofu Mkuu wa Kanisa la PAG Bishop Daniel Awet alivyofungisha Ndoa ya Vijana Pastory Mathew na Salome Julius.. HONGERENI SANA

Vijana Pastory Mathew na Salome Julius walifunga Ndoa yao Takatifu hivi karibuni katika Kanisa la PAG Apa Kitete lililopo Karatu.
Mbali Ndoa kuwa na Baraka nyingi mno Baraka kubwa zaidi ilikuwa kuhudhuriwa na jopo la Maaskofu wa Kanisa hilo Taifa na jimbo. 
Maaskofu Wakielekea Karatu kwa ajili ya Hafla ya ndoa ya Vijana Pastory Mathew na Salome Julius. Kutoka Kulia anayeonekana ni Askofu Mkuu wa Kanisa la PAG Taifa Bishop Daniel Awet na kushoto anaendesha gari hilo ni Askofu wa Jimbo la Arusha Steven Gobre.
Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Taifa Bishop Daniel Awet Alisafiri kutoka Arusha hadi Karatu kwa zoezi moja la kwenda kufunga Ndoa ya Vijana hao halikadhalika Askofu wa Jimbo la Arusha Steven Gobre naye alihudhuria hafla ya Ndoa hiyo takatifu.
Askofu Mkuu wa Kanisa la PAG Taifa Bishop Daniel Awet akiwasili Karatu.
Kingine usichokijua katika ndo a hiyo ni kwamba Pastory Mathew ni kijana wa Mkuu wa Shule ya Bible School ya PAG Arusha ambaye pia ni mchungaji wa Kanisa la PAG Apa kitete.
Mchungaji Mathew William wa Kanisa la PAG Apa Kitete na baba Mzazi wa Bwana Harusi Pastory Mathew.
Shamra shamra nderemo zilijaa kwenye ndoa hiyo Waumini walijaa furaha tele kwanza kwa Vijana wao kufunga ndoa Takatifu ya kikristo na pili ujio wa Jopo hilo la Maaskofu wakuu na furaha nyingine ilikuwa kuwa Bwana Harusi Pastory Mathew ni mtoto wa Mchungaji Mathew William Amsi ambaye ndiye Mchungaji kiongozi wa waumini hao.
Hawa ni bibi zake Bwana Harusi Pastory Mathew ambao waliambatana na waumini kushuhudia ndoa hiyo ya Mjukuu wao.

VOA TV News & Habaritanzaniagracemacha.com haikuwa mbali kukuletea Updates zote kutoka wilayani Karatu.

Hapa chini Kuna Video kutoka VOA TV News Itazame.

0 Comments:

Post a Comment