Friday, May 12, 2017

TAHADHARI: Barabara kuu Bukoba-Mwanza - Dar es salaam imekatika , Magari kuzungukia mbali , Ufinyo wa barabara nayo kero tena , Hofu yatanda


Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, barabara kuu ya  Mwanza , Bukoba - Dar es salaam imekatika ktk eneo la Kemondo magari hayapiti.

Magari yote ya abiria na mizigo yanayoenda mikoani yanalazimika kuzunguka Kyetema kupitia Katerero na kutokezea mbele ya Kemondo na kuendelea na safari.

Hofu barabara inayotumika sasa ni finyu na magari ni makubwa na mengi yanayopita kuelekea nje ya nchi kupitia mpaka wa Mtukula kwenda Uganda.

Lakn pia barabara yanakopita kuna tundu katika karavati moja hali inayoweza kusababisha hata barabara hiyo kukatika na kukosa pa kupita.

No comments:

Post a Comment