Friday, May 12, 2017

HABARI: Gambo Apokea zaidi ya Million 215 kama michango kwa tukio la msiba ulioisibi taifa hivi karibuni,


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema wameshapokea fedha za msaada zaidi ya shilingi milioni 215 kutoka kwa taasisi za umma, watu na taasisi binafsi  ambapo wameshatumia kiasi cha shilingi milioni 190.

Alisema fedha hizo zimegharamia  kusafirisha miili ya watoto waliofariki na walionusurika kutoka Karatu kuwaleta hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwa magari madogo.

Aidha fedha hizo zimetumika  kununua majeneza, kuandaa shughuli ya kuwaaga rasmi uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kusafirisha miili mpaka maeneo walikozikwa.
Alisema familia 32 za wanafunzi waliofariki kila moja imepatiwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 3.805.00

No comments:

Post a Comment