MAREKANI: Rais Trump asaini mkataba wa ushirikiano wa kiulinzi kati ya Marekani na Saudia , Dola Millioni 11 kutumika kuimarisha usalama wa kijeshi

Rais Trump akikagua Gwaride alipowasili Saudi
Akiwa katika ziara ya kikazi nchini Saudi Arabia Rais Trump amesaini deal la uimarishaji wa usalama katika ukanda huo ambapo zaidi ya dola za kimarekani million 11 zitatumika kuwafunza wanajeshi wa ulinzi wa Saudia na Marekani.

Rais Trump alifanya Ziara hiyo kukutana na viongozi wa umoja wa nchi za kiarabu United Arab Emirates ambapo aliungana nao katika mkutano maalumu wa viongozi hao wa kiislamu.Mkutano ulikuwa mahususi kwa ajili ya UAE na Marekani.


Pamoja na Mambo mengi yaliyozungumzwa ni pamoja na mkataba wa usalama wa eneo la mashariki ya kati ,Israel na Palestine.  Rais Trump ameahidi kuwa nchi yake chini ya usimamizi wake haitavunja uhusiano wake na UAE ili kulinda Amani na uimara wa uchumi katika ukanda wa mashariki ya kati.

Katika ziara hiyo Trump alikuwa pia aonane na Rais wa Sudan Omar All Bashir kwa mazungumzo kadhaa , harakati ambazo hazikuzaa matunda Baada ya Rais hiyo wa Sudan Omar Albashir kutotaka mazungumzo na Trump.

Ikumbukwe Rais Omar alikuwa akitafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za uhalifu wa hali za kibinadamu nchini Sudan.

0 Comments:

Post a Comment