MAREKANI: Rais Trump alaumiwa kwa kutotaja taifa la Palestina

Related image
Rais Trump
Rais Donald Trump inawezekana anajiamini anaweza kusaidia kusuluhisha makubaliano ya kihistoria kati ya Israeli na Palestina, lakini usimuulize utaratibu huo utachukua muelekeo gani kwa sababu inavyoonekana hatoelezea hilo.
Lakini kusita kwa Trump hata kutaja wazo la kuwepo taifa la Wapalestina kuna hatari ya kupelekea hisia hasi huku hali ikiwa tete Mashariki ya Kati, wakati Ikulu ya White House ikijaribu kuanzisha upya mazungumzo ya amani.
Pia inaweza kupelekea kuwepo kinyongo kati ya Wapalestina wengi kwamba Marekani sio msuluhishi muadilifu katika mgogoro kati ya Israeli na Palestina.
Lakini maafisa wa Marekani wanasisitiza kuwa Trump hapingi kuwepo kwa mataifa mawili; wanasema kuwa kwa ufupi anaweka njia zote mbadala wazi na kuwaruhusu Waisraeli na Wapalestina kujiamulia wenyewe ni vipi wanataka mazungumzo ya amani yachukue mkondo wake.
Wakati wa mkutano wake wiki hii na Kiongozi wa Palestina Rais Mahmoud Abbas, Trump alirejea kusema anamatumaini kufikia “makubaliano,” “mkataba” au kwa ujumla mwafaka wa namna fulani utakaopelekea “amani” kati ya pande hizo mbili hasimu.
Kitu cha wazi kilichokuwa kinakosekana kutoka katika maoni ya Trump ni kuligusia suala la suluhisho la kuwa na mataifa mawili, au fikra ya kuwepo taifa la Wapalestina, ambalo Marekani kwa kipindi kirefu imekuwa ikiona kama ndio njia bora ya mazungumzo ya amani juu ya Mashariki ya Kati.
“Alihakikisha kuwa kamwe hataji Palestina – uliona hilo, sawa?” Hanan Ashrawi, mwanachama wa Kamati ya Utendaji ya PLO ameiambia Sauti ya Amerika (VOA) ya Marekani .
“Nafikiri kwa namna fulani anajipurukusha kuacha kuizungumzia sera ya muda mrefu ya Marekani ya suluhisho la mataifa mawili.”

0 Comments:

Post a Comment