KIMATAIFA: Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vyaripoti kuhusu ushindi wa Moon

Kutoka NHK.

Kituo cha habari kinachoendeshwa na serikali ya Korea Kaskazini kimeripoti juu ya ushindi wa Moon war Korea Kusini siku mbili baada ya uchaguzi.


Jana Alhamisi Kituo Kikuu cha Televisheni cha nchi hiyo kimeripoti kuwa Moon Jae-in wa chama cha Democratic alipata asilimia 41 ya kura na kuchaguliwa kuwa rais wa 19 wa nchi hiyo. 

Taarifa hiyo haikujumuisha maoni mengine kuhusiana na matokeo hayo.

Kabla ya uchaguzi huo, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vilikuwa vikiashiria kuunga mkono serikali inayopendelea maafikiano nchini Korea Kusini.

Korea Kaskazini imeendelea kuwa kimya tangu Moon alipotoa maoni juzi Jumatano kuwa ataweza kuitembelea Korea Kaskazini hali itakaporuhusu.

0 Comments:

Post a Comment