Amiri jeshi mkuu wa Jeshi la Uturuki Hulusi Akar, msemaji wa rais Ibrahim Kalın, mkurugenzi wa idara ya upelelezi Hakan Fidan wamejielekeza mjimi Washington kabla ya ziara rasmi ya rais Recep Tayyıp Erdoğan nchini Marekani.
Rais Erdoğoan anatarajiwa kuwasili nchini Marekani ifikapo Mei 15.
Rais Erdoğan atafanya ziara ya siku 3 nchini Marekani ambapo masuala tofauti yatazungumziwa katika mkutano wao.
Masuala yatakayozungumzia ni pamoja na mzozo wa Syria na Iraq.
Vile vile kutazungumziwa suala la kumrejesha kiongozi wa kundi la wahaini wa FETÖ Fetullah Gülen ambae anatuhumiwa moja kwa moja kuhusika na jaribio la mapinduzi la Julai 15 mwaka 2016 nchini Uturuki.
No comments:
Post a Comment