Saturday, May 6, 2017

ISIS; , Magaidi 350 raia wa Uingereza warejea nyumbani kutoka Syria

Mashirika ya kijasusi ya Uingereza yameonya kuwa raia 350 wa nchi hiyo ambao ni magaidi wanachama wa kundi la kigaidi la ISIS wamerejea nchini humo kutoka Syria na sasa ni tishio kubwa kwa usalama.
Maafisa wa usalama wanasema magaidi hao sugu ambao waliondoka Uingereza na kujiunga na kundi hilo la wakufurishaji wamekuwa wakitarajiwa kurejea nyumbani kwani ISIS imekuwa ikipata pigo Syria na Iraq na hivyo kupoteza ardhi ambazo ilikuwa imezikalia kwa mabavu.
Mashirika ya usalama  Uingereza yanasema ni vigumu kufuatilia kila gaidi aliyerejea kwani idadi yao ni kubwa na wanarejea kwa mpigo.
Hayo yamedokezwa huku kukiimarishwa usalama katika nchi hiyo ya Ulaya baada ya kujiri shambulizi nje ya jengo la bunge mjini Laondon hivi karibuni ambapo watu wanne walipoteza maisha  wakati gaidi  mmoja aliendesha gari kiholela na kuwagonga wapita njia huku akimdunga kisu polisi.
Gaidi maarufu wa ISIS aliyejiita 'Jihadi John' alikuwa raia wa Uingereza na inasemekana aliuawa Novemba 2015
Serikali ya Uingereza inasema raia 800 wa nchi hiyo wako nchini Syria na Iraq  ambako wamejiunga na kundi la kigaidi la ISIS na wanahesabiwa kuwa tishio kwa usalama wanaporejea makwao.
Mwezi Februari, Polisi ya Ulaya, Europol, ilitangaza kuwa magaidi 5,000 wa ISIS sasa wako Ulaya na kwamba kwa ujumla kuna magaidi 30,000 kutoka nchi 100 duniani ambao wamesafiri Syria na Iraq tokea mwaka 2011 na kujiunga ma makundi ya kigaidi nchini humo. SOURCE HERE

No comments:

Post a Comment