KIONGOZI WA N. KOREA |
Korea Kaskazini imeyashutumu mashirika ya kijasusi ya Marekani na Korea Kusini kwa kutuma makundi ya kigaidi nchini humo kwa lengo la kumuua Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.
Wizara ya Usalama wa Taifa ya nchi hiyo ilitoa taarifa kupitia shirika la habari linaloendeshwa na serikali jana Ijumaa. Ilisema Shirika la Kijasusi la Marekani-CIA kwa kushirikiana na Shirika la Usalama wa Taifa la Korea Kusini, yalimuhonga mfanyakazi raia wa Korea Kaskazini nchini Urusi ili amuue Kim kwa kutumia silaha za kemikali.
Taarifa hiyo ilisema Korea Kaskazini ililibaini kundi la kigaidi lililoingia kinyemela nchini humo. Taarifa hiyo imeonya kuwa shambulio la kukabiliana na ugaidi litatekelezwa ili kuwateketeza majasusi hao na mashirika yaliyohusika na mipango hiyo ya Marekani na Korea Kusini.
Ukweli juu ya taarifa hiyo bado haujathibitishwa lakini wachunguzi wa mambo ya Korea Kaskazini wamedai kuwa huenda hatua hiyo inalenga juu ya kuongezeka kutolewa kwa wito nchini Marekani kuijumuisha tena Korea Kaskazini katika kundi la mataifa yanayofadhili ugaidi.
Bunge la Wawakilishi la Marekani limepitisha muswada unaoutaka utawala wa Rais Donald Trump kuirejesha Korea Kaskazini kwenye orodha hiyo.
No comments:
Post a Comment