HABARI: Ni kuhusu Korea Kaskazini tena , leo UNSC INAIJADILI KOREA KASKAZINI visa vya makombora , Udukuzi wa mtandaoni nao ni mada katika mjadala wao

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa-UNSC wamekubaliana kuziomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutekeleza kwa ukamilifu maazimio ya vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.

Kikao hicho cha ndani cha dharura kilifanyika jana Jumanne kujadili jaribio la hivi karibuni la urushaji kombora lililotekelezwa na Korea Kaskazini.

Rais wa UNSC ambaye pia ni Balozi wa Uruguay kwenye Umoja wa Mataifa, Elbio Rosselli, aliwaambia waandishi wa habari kuwa nchi hizo wanachama pia zilikubaliana kutovumilia mpango wa uendelezaji nyuklia na urushaji makombora wa Korea Kaskazini. Alisema baraza hilo liliiomba Korea Kaskazini kuanza kuchukua hatua kuondokana na silaha za nyuklia kwenye eneo la Rasi ya Korea. Rosselli hakuweka wazi iwapo hatua za ziada zitachukuliwa.

Kabla ya mkutano huo wa jana Jumanne, Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley, alisema Marekani inajadiliana kwa ukaribu na China juu ya kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini. Alisema upande wa China ulimjulisha juu ya nia yake ya kuchukua hatua iwapo Korea Kaskazini inakaribia kukamilisha uendelezaji wa makombora yanayovuka mabara.

Marekani na China zinatarajiwa kuendelea na majadiliano kwenye Baraza la Usalama juu ya iwapo iimarishe vikwazo.

Korea Kaskazini ilirusha aina mpya ya kombora la masafa ya kati kuelekea Bahari ya Japani Jumapili iliyopita. Kombora hilo aina ya Hwangsong-12 linaaminika kuruka kufikia umbali wa zaidi ya kilomita 2,000 kutoka usawa wa bahari.

0 Comments:

Post a Comment