Katibu wa kanda ya kaskazini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mhe.Amani Golugwa amefanya kikao cha ndani katika Jimbo la Longido Mkoani Arusha ambapo kikao hicho kiliudhuriwa na aliyekuwa Mbunge wa Longido Mhe.Onesmo Ole Nangole ,Viongozi, kamati Tendaji pamoja na wanachama wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
Pia katibu huyo wa Kanda ya kaskazini amewapokea wanachama wapya vijana kwa wazee waliojitokeza na kujiunga na CHADEMA na kuwapatia Kadi za uwanachama na bendera moja kwa kila mwanachama,amewaelekeza kuwa bendera izo ni kwaajili ya kutengeneza msingi katika sehemu wanayotoka.
Wanachama hao wapya walipokea maelekezo hayo kwa shauku kubwa na wameahidi wanaenda kulifanyia kazi swala hilo kwa weledi mkubwa kabisa,ili atakapo rudi Longido aje afungue misingi hiyo rasmi.
M/Kiti wa CHADEMA mkoani Arusha Amani Golugwa akimkabidhi Kadi ya CHADEMA |
Wanachama hao wapya walipokea maelekezo hayo kwa shauku kubwa na wameahidi wanaenda kulifanyia kazi swala hilo kwa weledi mkubwa kabisa,ili atakapo rudi Longido aje afungue misingi hiyo rasmi.
No comments:
Post a Comment