BURUDANI LEO: Raymond (RayVanny) choice ya Laizer WCB Wasafi

Raymond RayVanny msanii Wa WCB-Wasafi
Kutoka Label inayoaminika zaid Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla WCB Wasafi nimekusogezea story inayomuhusu Produza nguli katika label hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Laizer ni Produza mwenye uwezo mkubwa ukilinganisha na hali ya ya soko la muziki lilivyo ambayo hutegemea sana kazi nzuri toka kwa Maproduza wabunifu zaidi.

Leo Laizer amemtaja msanii anayemuekewa zaidi wakati wakifanya projects za production ya muziki katika Label ya WCB ya Diamond. 

WCB Wasafi yenye wasanii 6 hafi hivi sasa imekuwa na sifa kubwa kwa kutengeneza wasanii na nyimbo Kali zinazokonga nyoyo za wengi. Wasanii wanaoiunda Label ya WCB Wasafi kwa sasa ni Queen Darleen, Harmonize, Rich Mavoko , Lava Lava , Raymond (RayVanny) na Diamond Platnumz a.k.a Simba 

Produza Laizer amesema msanii Raymond (RayVanny) ndiye msanii ambaye ni Wa kipekee katika Label hiyo ambaye anaelewa jinsi Track Kali inavyokaa na mini Produza Laizer anataka. 
Produza Laizer Wa Label ya WCB Wasafi
"Msanii yoyote anayejua mimi nina enjoy sana kufanya naye kazi, ukimuelekeza fuata hiki anafuata lakini naweza kusema kwa kuwa Raymond ndiye msanii aliyegundua kitu kilichopo ndani ya Lizer huwa nina enjoy naye zaidi kwasababu ndiye msanii ambaye nilitoka naye.” Amemuambia mtangazaji wa Ice Fm, ya Njombe, Gami Dee.

Endelea kubaki nami ikiwa ni pamoja na kwenye Mitandao ya kijamii Facebook ,Twitter, Instagram,  kote kwa jina la Habari Tanzania Grace Macha  bila kusahau kutazama Latest Videos zote katika V.O.A TV YouTube.

0 Comments:

Post a Comment