UPDATES: Korea Kaskazini Inasema urushwaji Wa Kombora jipya uliongozwa kwa usahihi , Kim alisimamia zoezi hilo.




Chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali ya nchi hiyo leo Jumanne asubuhi kilisema kuwa jaribio hilo lilitekelezwa chini ya usimamizi wa Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo, Kim Jong Un.


Gazeti la Rodong Sinmun la Chama cha Wafanyakazi limechapisha picha 18 za kile lilichodai kuwa ni kombora jipya pamoja na picha za Kim Jong Un kwenye ukurasa wa kwanza na wa pili wa toleo la leo Jumanne.

Picha hizo zinaonesha kombora hilo likiruka kutoka kwenye mtambo wa kurushia makombora unaohamishika huku likitoa miale ya moto na kuendelea kuruka juu angani. Kim Jong Un anaonekana kutabasamu na kunyooshea kidole kwenye skrini inayoonekana kuonesha data za urukaji wa kombora hilo.

Kim Jong Un ameripotiwa kuridhishwa kuwa mchakato wa maandalizi ulikuwa wa kisasa zaidi na kuiwezesha nchi hiyo kujiandaa kuwashinda maadui zake kwa haraka zaidi.

Korea Kaskazini imedai kuwa kombora hilo lilianguka ndani ya mita saba za eneo lililokusudiwa.

Ripoti hiyo huenda inahusu jaribio la urushaji wa kombora lililoonekana kuekelezwa jana Jumatatu jirani na mji wa Wonsan mashariki mwa nchi hiyo.

Serikali ya Japani inakadiria kuwa kombora hilo lilianguka kwenye eneo la maji ndani ya ukanda maalum wa kiuchumi wa Japani kwenye Bahari ya Japani, takribani kilomita 300 kutoka kwenye mtungo wa visiwa vya Oki, mkoani Shimane.

0 Comments:

Post a Comment