Mgogoro uliopo hivi sasa kati ya Tanesco na
IPTL unahusu kiwango cha malipo ya
uwekezaji yaani capacity charges ambacho
IPTL walikuwa wanalipwa na Tanesco.
Wakati haijafahamika nani aliyelipwa
mabilioni ya shilingi yaliyokuwa kwenye
akaunti ya Escrow katika Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), kutokana na mvutano baina
ya Tanesco na Kampuni ya IPTL, imebainika
kuwa Bunge liliwahi kuagiza fedha hizo
zisichukuliwe mpaka mitambo ya IPTL
itakapokuwa chini ya Tanesco mwakani.
Hiyo imo katika taarifa ya iliyokuwa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika
ya Umma (POAC), kwa mwaka wa fedha
ulioishia Juni 30, 2007.
Hata hivyo, Gavana wa BoT, Profesa Benno
Ndulu alithibitisha jana kuchotwa kwa Dola za
Marekani 122 Milioni (Sh195.2 bilioni) katika
akaunti hiyo, lakini akakataa kutaja nani hasa
aliyelipwa.
▼
No comments:
Post a Comment