Baada ya katibu mwenezi wa Njombe mjini
na mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm Taifa
ndugu Evaristo Lupenza kutangaza kujitoa
katika chama hicho na kuacha madaraka yake
yote aliyokuwa nayo kuanzia ngazi ya kata
hadi taifa.Leo kada mwingine anayeaminika
kwa mipango ya uchachuaji wa kura ndugu
Gerald Mwalongo A.K.A Magaga amejivua
rasmi nyadhifa zote alizokuwa ndani ya
chama hicho.Bwana Magaga alikuwa ni
mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya wazazi
wilaya pia mtaalamu wa mambo ya ufundi
ndani ya chama hicho katika wilaya ya
Njombe ameamua kuachana na chama hicho
kutumika kama kiongozi.
Kujitoa kwa Bwana Magaga ni pigo kubwa
sana kwa chama kizee hapa Njombe.Bwana
huyu kama ni mpira basi huyu ndiye
aliyekuwa na sifa ya kushika ndumba.Kwa
Njombe hakuna mbunge au diwani ambaye
hakufika nyumbani kwa huyu Bwana na
kukata kitu kidogo.Alikuwa ni zaidi ya
mwanachama wa ccm.
Kujiondoa kwa hawa makada wawili wa ccm
ni dhahiri Njombe sasa kama CHADEMA
wakijipanga vizuri wanaweza kuwa na nguvu
sawa na mikoa mingine yenye nguvu kama
Arusha,Mbeya,Mwanza n.k.
Leo karibu siku nzima viongozi wa chama cha
mapinduzi wameshinda wanahangaika
kunusuru hali ya makada wake kujitoa.Diwani
wa viti maalum anayekaa jirani na Highland
Hotel akishirikiana na katibu wa ccm wilaya
wameshinda wanahangaika kukutana na
makada ambao wameingia kwenye mgogoro
mkubwa wa kutuhumiana juu ya fedha za
kampeni za udiwani uliofanyika Njombe mjini
tarehe 9.2.2014 ambapo pamoja na kampeni
za chama cha mapinduzi kuwahusisha
wanasiasa wengi wenye majini kama
Mwakyembe,mwigulu,Deo Filikudzombe,Jah
people(Deo Sanga),Ana Makinda,Deo
Mwanyika na wengine wengi bado
waliabishwa na CHADEMA walioshinda kwa
kura nyingi sana.
katika uchaguzi wa Njombe kila kada
alikabidhiwa fungu la kugawa kwa wananchi
ili kuwashawishi wawapigie kura ccm.Mwisho
wa yote inasadikika Makada wapenda
mabadiliko waliamua kuzibana fedha zote na
kufanyia mambo yao binafsi na hivyo
kushindwa hata kufanya tathmini baada ya
uchaguzi.
Hadi mwisho wa uchaguzi unamalizika
makada waliobaki kwenye mapambano ni
Ngole ambaye aliishia kupata kichapo cha
nguvu toka kwa makada wa chadema
waliofanikiwa kumkamata na kumbana
'KUNAKO'kitu kinamsababishia kuendelea na
matibabu hadi leo na inawezekana eneo hilo
nyeti limeharibiwa vibaya na kugharimu
maisha ya viotea.
Jah people naye pamoja na unene alifanikiwa
kutoroka kukwepa nguvu ya umma.
▼
No comments:
Post a Comment