Niko kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga kufatia kifo cha aliyekuwa mbunge na waziri wa fedha mhe Mgimwa msemaji mkuu ni Mhe. Freeman Mbowe...nitawaletea ktakacho kuwakikiendelea pamoja na picha za matukio mbalimbaili........
Anasema Chadema imefanya kampeni za kila aina. Anatoa ushuhuda namna
ambavyo yeye ni mfano wa kukataa mfumo wa kurithishana ubunge.
Wananchi huko Kidamali wamemzomea mgombea wa CCM amempandisha jukwaani
mke wake mzungu anaitwa Robbie. Wananchi wamezomea na kucheka sana.
Nassar anapiga nondo za Arumeru, chopa hiyooooo inakatiza hapa umati
unalipuka.
Mbunge mtarajiwa huyo katua hapa.
Sugu anasema wabunge wamekuja kukomaa hapa kwa sababu Grace ana uwezo.
Anaeleza historia yake alivyokuwa mtu wa kawaida tu akaenda kuwa mbunge.
Hakuwa mbunge kwa sababu baba yake alikuwa mbunge. Anawataka wananchi
kesho watume ujumbe kwa watawala kwamba hilo halikubaliki. Alichokuwa
nacho Mgimwa mkubwa hakiwezi kuhamishiwa kwa mtoto hats kidogo. Uchaguzi
huu si wa Kalenga pekee...

No comments:
Post a Comment