▼
Saturday, March 15, 2014
Uzinduzi wa kampeni za CCM Chalinze wadoda..
Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM Chalinze umedoda.Hamasa kubwa iliyofanywa kwa kutumia magari ya matangazo na mashangingi imepata mwitikio mdogo.Mbaya zaidi Mvua kubwa inanyesha muda huu na kuzima kabisa ndoto ya kupata wahudhuriaji angalao wachache wa kusikiliza hotuba za ufunguzi.CCM wanafanya mkutano wao eneo la Miono ambapo ni nyumbani kwa Mbunge aliyetangulia Said Bwanamdogo.Wazigua na wa Kwere wenye msimamo wa wastani wamesusia mkutano huu kwa kuwa hawaridhishwi na mazingira ya kifo cha Mbunge wao ambaye anaaminika kuwa alifanyiwa hujuma kwa sababu za kisiasa ili mtoto wa mwenyekiti wa chama arithi jimbo aliloshikilia baba yake kwa sasa kabla ya baba yake kuondoka madarakani.Pia hoja kubwa ni kuwa baba yake mgombea wa CCM alikua Mbunge kwa muda mrefu na hakufanya kitu,iweje Said Bwanamdogo aliyejitahidi miezi 12 ya kwanza kufanya kazi za maendeleo akwamishwe na wakubwa na kisha kumuondoa kabisa duniani halafu leo aibuke mtoto wa Mwenyekiti na kutoa ahadi kuwa atamalizia ahadi za Marehemu Said BwanaMdogo? Wazigua na Wakwere wenye msimamo wa wastani wanasema hii ni laana kwa mujibu wa mila na tamaduni zao.
No comments:
Post a Comment