Wednesday, December 4, 2024

Waliotaka Kumteka Tarimo Wanaswa na Jeshi la Polisi



Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata wahalifu wanane waliojaribu kumteka mfanyabiashara,  Deogratius Tarimo, katika tukio lililotokea tarehe 11 Novemba 2024, eneo la Kiluvya, Ubungo, Dar es Salaam. 


Polisi wamefanikiwa kukusanya ushahidi muhimu na kupitia uchunguzi wa kina, waligundua kuwa kundi hilo la wahalifu lilikuwa linapanga njama za kumteka na kumdhuru Tarimo.



Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Muliro Muliro – SACP, wahalifu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Dar es Salaam, Songea (Ruvuma), na Mbingu (Mimbo) Morogoro, baada ya uchunguzi wa kisheria na ufuatiliaji wa karibu. 


Polisi pia walipata gari aina ya Toyota Raum, ambalo lilitumika katika tukio hilo, likiwa na namba isiyo halisi T 237 EGE, lakini baada ya uchunguzi walibaini kuwa namba halisi ya gari hiyo ni T 237 ECF.


Waliokamatwa kwenye tukio hilo ni pamoja na:


1. Bato Bahati Tweve, Miaka 32, Mkazi wa Kimara Bunyokwa na Songwe Mbozi

2. Yusuph Abdallah, Miaka 32, Mkazi wa Mbingu

3. Fredrick Juma, Miaka 31, Mkazi wa Kibamba

4. Nelson Elimusa, Miaka 24, Mkazi wa Mbezi Luguluni

5. Benk Daniel Mwakalebela, Miaka 40, Mkazi wa Mbezi Makabe na Kyela, Ipinda

6. Thomas Ephraim Mwakagile, Miaka 38, Mkazi wa Bunyokwa na Kyela Ngonga

7. Anitha Alfred Temba, Miaka 27, Mkazi wa Mbezi Mwisho

8. Isack Mwaifani, Miaka 45, Mkazi wa Kinyerezi


Kamanda Muliro amesema kuwa operesheni hii ni sehemu ya juhudi za kudhibiti na kuzuia vitendo vya kihalifu, na kwamba wahalifu hao watachukuliwa hatua kali za kisheria. 


Aidha, jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa muhimu ili kuzuia matukio ya kihalifu kabla hayajatokea.



No comments:

Post a Comment