Viongozi wa CHADEMA Lissu, Mnyika, Sugu Wakamatwa Mbeya








Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewakamata viongozi wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Taifa, Tundu Lissu. Viongozi hao walikuwa wakifanya kikao cha ndani katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyasa wakati wa kukamatwa kwao.



Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, viongozi hao walikuwa mkoani Mbeya kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Vijana Kitaifa kwa Chama hicho jijini Mbeya.



Msemaji wa CHADEMA, Jon Mrema, amethibitisha kwamba viongozi waliokamatwa ni pamoja na Lissu, Katibu Mkuu John Mnyika, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi, na viongozi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Vitus Nkuna.



Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na agizo la Kitaifa la Jeshi la Polisi ambalo limepiga marufuku mikusanyiko ya kisiasa ya CHADEMA kwa madai ya kuwa na viashiria vya kuvuruga amani ya nchi 

0 Comments:

Post a Comment