RAIS, Samia Suluhu Hassan ameikaribisha ikulu Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake chini ya Umri wa Miaka 17 ( Serengeti Girls) chakula cha mchana ikiwa ni muendelezo wa pongezi zake kwa timu hiyo baada ya Kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini India.
Viongozi wa Serikali na Mpira wa Miguu wakiongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbas na wengine wamehudhuria tukio hilo lililofanyika leo Julai 05, 2022 Ikulu Dar es Salaam.
Hafla hiyo, imepambwa na Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya akiwemo Barnaba na Frida Amani.




No comments:
Post a Comment