Wednesday, May 11, 2022

MDEE NA WENZAKE 18 WATINGA MLIMANI CITY KUSIKILIZA RUFAA XAO


WALIOKUWA wanachama wa Chadema, Halima Mdee na wenzake 18 wamefika kusikiliza rufaa zao katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kunakofanyika kikao cha Baraza kuu la CHADEMA.



Kikao hicho kinafanyika leo Mei 11, 2022 na kinakadiriwa kuhudhuriwa   na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho, wanaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema Baraza Kuu litakuwa na ajenda 11 ambayo ni mpango mkakati wa chama kwa miaka tano pamoja na mpango kazi wa mwaka.

Mrema amesema ajenda nyingine itakuwa ni rufaa ya nidhamu iliyokatwa na wabunge 19 wa viti maalumu wakiongozwa na Halima Mdee wakipinga kuvuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho iliyoketi mwisho mwa mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment