"Nisisahu kujitambulisha kwenu kuwa, mimi ndiye Rais wa Uganda ambaye nilichaguliwa na watu wa Uganda"
"Pamoja na kuwa katika maeneo tofauti ya kijiografia lakini mambo tunayoyapitia katika siasa yanafanana"
"Kwa mara ya kwanza ilibidi mgombea urais nchini Uganda katika uchaguzi mkuu nchini humo kuvaa kifaa cha kuzuia risasi, na ni uchaguzi uliomwaga damu nyingi za raia wema"
"Timu yangu ya kampeni iliyokuwa na watu takribani 130 walizingirwa na kukamatwa na kukaa jela kwa miezi 7. Pamoja na mazingira hayo yote ulikuwa ni uchaguzi ambao watu wa Uganda walishinda"
"Nawapa salamu kutoka kwa watu wa Uganda, ambao hawajakata tamaa na hawataacha kupaza sauti kwa mambo ambayo hayaendi sawa. Nadhani hilo halina tofauti sana na hapa Tanzania"
"Baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 najua kuna watu wengi hususan wa chama cha CHADEMA walikamatwa na kuteswa"
"Tunakutana hapa wakati Makamu Mwenyekiti wa@ChademaTz Bara, @TunduALissu yuko uhamishoni, na hizo ndio changamoto amazon tunazipitia. Ni muhimu kusimama kwa pamoja kukaa na kuona tunatatua vipi changamoto za namna hii"
"Tusiangalie mateso yetu au pale ambapo tutakuwa tumeumia, bali tuangalie matumaini yaliyopo mbele yetu"
"Kwa kuwa tumezikubali na kuzielewa changamoto zinazotukabili, tumeamua kuja na mkakati wa ushirikiano wa pamoja ili kuweza kuzitatua"
"Pale ambapo tunapata changamoto, njia ya kutatua changamoto hizo ni kuwa wamoja na kukaa pamoja, hata wazee wetu walipokuwa wanapambana na ukoloni, pindi walipopata changamoto walikutana na kuungana na kisha kutatua changamoto hizo"
"Kama hauwezi kujifunza kwa yaliyotokea huko nyuma, huwezi kutengeneza njia nzuri huko mbele unapokwenda"
"Wakati Rais Yoweri Museveni anachukua madaraka kwa mara ya kwanza, mimi (Bob Wine) nilikuwa nina miaka minne, na sasa nina miaka 40 huku Rais Museveni akiwa hana mpango wa kustaafu"
"Wote tunaamini katika mazungumzo, lakini mazungumzo kule kwetu (Uganda) ni 'kitu gani unataka'."
"Kitu kikubwa katika siasa ni watu, kupitia watu kila kitu kitafanyika na kila kitu kitasemwa. Kila kitu kitachofanywa tuhakikishe kinawahusu watu"
"Pamoja na madhaifu ya Rais Museveni, lakini Katiba ya Uganda ni nzuri, lakini tatizo ni moja tu katiba yetu (katiba ya Uganda) haiheshimiwi"
"Nguvu ya umma ina nguvu kuliko watu wote walioko madarakani. Sisi Wakiristo tunafundishwa kuwa suati ya wengi ni sauti ya Mungu"
"Tuendelee kumuamini Mungu, kwani Mungu anatenda miujiza. Wakati tunapoendelea kusubiria hiyo miujiza tuendelee kupambana kwa pamoja"

No comments:
Post a Comment