Wednesday, April 27, 2022

KINANA ; WATUMISHI WA UMMA WANAOTAJWA RIPOTI YA CAG WACHUKULIWE HATUA


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Tanzania Bara komredi Abdulrahman Omar Kinana ameishauri  serikali kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wale wote waliotajwa kwenye ripoti ya mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa hesabu za serikali (CAG).



Ameyasema hayo leo April 27, 2022  kwenye mkutano wa ndani wa chama hicho jijini Arushaa akiambata na Katibu Mkuu wa chama hicho Danuel Chongolo, katibu wa NEC itikikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka

 

“Wakati umefika kwa serikali kuchukua hatua kwa wahusika wote waliotajwa kwa kuisababishia serikali hasara, upotevu au ubadhirifu wa fedha za umma kupitia ripoti ya CAG,” amesema Kinana na kuongeza


... Ripoti ile inaonesha mambo ya hovyo yamefanyika, Si uzushi kazi ile ya ukaguzi imefanywa kisayansi na kitaalamu, wabunge wameijadili kwa ukali sana, hata wasomi na wananchi wengine wameijadili kwa ukali vile vile,"

" Mimi nadhani ingekuwa vyema hatua ziwe zinachukuliwa papo kwa papo ili watu wajenge nidhamu na heshima kwa fedha za wananchi,” .


Kinana  alisema pamoja na kwamba hana mamlaka ya kutoa amri kwa serikali lakini atamwambia Rais juu ya ushauri huo.


“Kwa nafasi yangu nazungumza kwa niaba ya mwenyekiti wetu ambaye ni Rais kwamba wahusika wachukuliwe hatua. Si kila jambo lazima Rais aagize, tujenge utamaduni wa kuwajibika sisi wenyewe," amesema Kinana.


Amesema lazima kuwe na utaratibu wa kuwajibika mtu anapofanya kosa na akishindwa kufanya hivyo vyombo na taasisi zenye wajibu wa kusimamia uadilifu kwa viongozi na watendaji nchini hususani kwenye kujenga nidhamu na fedha za umma zichukue dhidi yake.


“Tujenge utamaduni wa kuwahi kuchukua hatua kwa wakati, mtu akae pembeni apishe uchunguzi na akithitika apishe wengine kwani kuna watu wengi wana uwezo hawana kazi," amesema Kinana na kuongeza


... Kila ripoti ya CAG inapotolewa tukianzia na hii wale wanaotajwa wawajibishwe kujibu na kuchukuliwa hatua. Ikiendelea kubaki hivi, ripoti inatolewa na kuwekwa kabatini fedha za wananchi zitaendelea kuchezewa.”.


 Kinana amehitimisha ziara yake ya mikoa minne ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha ya kukagua uhai wa chama.

No comments:

Post a Comment