Thursday, March 31, 2022

ZAINA FOUNDATION YAWANOA WAANDISHI WANAWAKE ARUSHA



WANAWAKE wengi wamekuwa hawana uelewa mpana kuhusiana na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii (social Media) jambo linalowafanya wakati mwingine kujikuta ni wahanga ya udhalilishwaji mitandao.


Mkurugenzi wa taasisi ya Zaina foundation, Zaituni Njovu ameyasema hayo  wakati akitoa mafunzo ya siku mbili ya usalama mtandaoni kwa wanahabari wanawake mkoani Arusha ili kuwawezesha kutekeleza majuku yao kwa ufanisi zaidi.

Amesema wanawake wengi bado hawajatambua matumizi sahihi ya hii mitandao hii ya kijamii,ni namna gani watumie mitandao katika mawasiliano ambayo yana tija katika maisha yao.

"Sisi kama Zaina Foundation tuliona kwamba kwa wanawake kuna upungufu mkubwa wa kuelewa umuhimu wa mtandao hawajui matumizi sahihi ya mitandao katika kazi zao ikiwemo katika biashara zao ,elimu ,uchumi biashara na mawasiliano yenye tija katika biashara zao wanawake wengi yale mauthui ambayo wanayatuma katika mitandao yao ya kijamii bado ubora wake upo chini ukilinganisha na makundi mengine," amesema Zaina.


Amesema wanawake wengi wamekuwa wanapeleka maudhui ambayo baadae yanakuja kuwatafisiri vibaya au yana wahukumu na wakati mwingine kujikuta wapo katika swala la ukatili wa kijinsia mtandaoni.


Zaina amesema mpaka sasa wameshatoa mafunzo kwenye mikoa ya  Dar es salaam, Arusha, Tanga na Mtwara  ambapo wanampango wa kuendelea kutoa elimu ya usalama mtandaoni kwa wanawake kwenye mikoa yote nchini.




No comments:

Post a Comment