Friday, March 25, 2022

NTC ARUSHA WAIOMBA OFISI YA RAS IWASAIDIE KUPATA ENEO LA KUJENGA MABWENI

 

 

  


CHUO cha Taifa cha Utalii, (NTC) tawi la Arusha wameiomba ofisi ya Katibu Tawala mkoani Arusha, (RAS), Athuman Kihamia kuwasaidia kupata ardhi kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kwenye eneo lililopakana na chuo hicho.

 


Ombi hilo limetolewa leo Machi 25, 2022 na Mkuu wa chuo hicho Tawi la Arusha, Dkt Maswet Masinda, wakati wa mahafali ya vijana wanagenzi 111 waliogharamiwa mafunzo hayo na ofisi ya waziri mkuu ambapo mgeni alikuwa Katibu  tawala huyo.

 

Amesema kuwa tatizo kubwa linalowakabili ni ufinyu wa eneo huku akiainisha kuwa jirani yao ambaye  yupo kwenye hafla hiyo analo eneo kubwa ambalo halijaendelezwa  hivyo akaiomba ofisi ya RAS ione namna inaweza kusaidia waweze kupata eneo dogo la kujenga mabweni.

 

" Eneo kwa ajili ya madarasa na ofisi tunalo, lakini mabweni yanatakiwa yawe mbali kidogo na eneo la madarasa kwa hiyo mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa  chuo cha Taifa cha Utalii tunakuomba na tunaiomba ofisi yako kwa namna ya kipekee sana itusaidie kupata eneo hilo," amesema Dkt Masinda na kuongeza.

 

... Serikali imepania kuboresha na wadau wetu wa utalii wako tayari kutusaidia katika ujenzi wa hosteli kwa   ya ujenzi wa mabweni kwa ajili ya vijana wetu,".

 

Dkt Masinda amesema kuwa Wizara iliwapangia wanachuo 120 lakini  waliohitimu lel ni  111 ambapo wengine waliacha masomo kutokana changamoto mbalimbali lzilizowakabili ambazo  si  za kifedha kwa sababu walikuwa wanasoma bure.

 

"Wengine walipata kazi, waliajiriwa wakiwa masomoni wakapima wakaamua kuendelea na kazi badala ya kuendelea na mafunzo," amefafanua Dkt Masinda. 

 


Amesema kuwa hayo ni mafunzo kwa awamu ya tatu ambapo kwa NTC ni awamu ya kwanza kuwapokea jumla ya wanafunzi 140 ambapo kampasi ya   Arusha wamepokea wanafunzi 120  na 120 wengine  walipokelewa kwenye kampasi yao ya Bustani.

 

 

"Sasa tunaenda awamu ya pili, pia wizara imepanga kuongeza idadi, nitoe wito kwa vijana waweze kuzitumia hizi fursa.Wakati nafasi zilipotolewa kampasi ya Arusha ilipokea maombi 1,103 kati yao walichaguliwa ni 120," amesema Dr Masinda na kuongeza

 

"Tunaweza tukaona ni jinsi gani hitaji lilivyokuwa kubwa kwa Taifa kwamba vijana wanahitaji kusoma. Vijana wetu tunawaasa pale mnapopata fursa mzitumie vizuri kwani kuna wengi wanaohitaji kupata fursa hizo lakini wanazikosa,",

 


Kwa upande wake Katibu tawala mkoa wa Arusha, Kihamia akiongea na wahitimu hao amewaasa kuwa mafunzo waliyopatiwa kwa  miezi hii sita ikiwemo miwili katika mafunzo kwa vitendo anaamini wameshabobea kilichobaki ni wao kwenda kufanya kazi na kuwa waadilifu na waaminifu huku wakitumia weledi waliopewa hapo chuoni kwa kulitumikia Taifa .

 

"Mimi niwaombe vijana wangu ambao mmehitimu hapa leo na ambao hawapo hapa, muwekee mkazo sana uzalendo wa nchi yetu na uaminifu na uadilifu kwa sababu itasaidia kurahisisha utekelezaji wa mipango ya serikali," amesema Kihamia na kuongeza.

 

...Unaweza kuajiri vijana kadhaa baada ya muda unakuta tuhuma huyu kaiba hiki huyu kafanya hiki, huyu kamtukana bosi wake huyu kaenda kinyume na maadili yake.

 

...Kizazi cha miaka ya sasa kuanzia 35 kurudi chini kwa kweli…. Ila naamini licha ya mafunzo mliyopata ya utalii na ukarimu  

naamini wamewaandaa  tabia zetu zikae vizuri.

 

…Ili kuona kwamba hamfanyi yale mambo ambayo ni kinyume na maadili na kwa jinsi mnavyopendeza na kung'ara naamini na weledi tabia na mienendo yenu inang'ara,”.

 

 

Wanachuo waliohitimu chuoni hapo  waliwashukuru Ofisi ya Waziri Mkuu iliyogharamia mafunzo yao, mkuu wa Chuo, wakufunzi  kwa kuwafundisha na RAS kwa kukubali kuwa  mgeni rasmi kwenye mahafali yao.

 


" Shukrani zetu za dhati na z kipekee ziende ofisi ya Waziri Mkuu kwa ufadhili huu wa mafunzo kwa asilimia 100 kwa vijana wa Kitanzania bila ubaguzi wowote,” alisema mwanachuo huyo akisoma risala ya wahitimu na kuongeza.

 

“Kwa kipitia mafunzo haya kuna wenzetu wamenufaika kwa kupata ajira mara baada ya kumaliza mafunzo yao ya vitendo kwenye mahoteli na migahawa mikubwa jijini Arusha,”.

 

Kwa upande wake mhitimu, Fadhila Kitundu amesema kuwa anashukuru kupata mafunzo hayo anayoamini yamemfanya awe bora zaidi na mwenye kuweza kuhimili ushindani wa soko la ajira.

 

“ Naamini mimi ninasifa zote zinazohitajika na tabia yangu ni njema na itaonekana kwa jamii na wataweza kunitofautisha na vijana wengine,” amesisitiza Kitundu.

 

Kwa upande wake mhitimu mwingine, Lilian Lameck amesema anajisikia vizuri na  furaha kwa sababuaimeweza kupata ajira kupitia kozi hiyo.

 

“Nawakaribisha vijana wengine waje chuo cha utalii  kampasi ya ya  Arusha lakini pia wanaweza kwenda Mwanza au Dar es Salaam zilipo kampasi mbili,” amesisitiza Lilian.

 

Naye Lussa Melembuke ameishukuru ofisi ya waziri mkuu kwa kuwaambini lakini pia wakufunzi wa chuo cha Taifa cha utalii, Arusha kwa kuwaamini kwani haikuwa rahisi kupenya kwenye kundi la vijana zaidi ya 1000 waliokuwa wakiwania nafasi hizi 120 

 

“Tunaahidi tutaendelea kupambana kutimiza ndoto zetu lengo ni kujiajiri au kiajiriwa Taifa liendelee kinufaika na uwepo wetu.” Smediditixs Melembuke.

 

 

Agosti mwaka jana Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alinukuliwa akisema Tanzania nzima kuna vijana takribani 45,000 ambao wamesambazwa katika vyuo vyote vya Serikali na vya binafsi ambapo watapatiwa mafunzo ya ufundi stadi kwa miezi sita kwa kugharamiwa na serikali.

 

No comments:

Post a Comment