MAHAKAMA ya Haki ya
Afrika Mashariki, (EACJ) imeielekeza serikali ya Tanzania kurekebisha sheria yake
ya vyama vya siasa kwani inakiuka vifungu vya mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika,(EAC).
Uamuzi huo umetolewa leo
Machi 25, 2022 na majaji watano akiongozwa na , Jaji Mfawidhi , Yohane
Masara, Jaji Mfawidhi Msaidizi, Audace Ngiye, na Majaji Charles Nyawello,
Charles Nyachae na Richard Wejuli.
Shauri hilo namba 3/
2020 lilifunguliwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa Taifa, CHADEMA,
Freeman Mbowe, aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo marehemu
Sharif Hamad, Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zito Kabwe, Mwenyekiti
wa Chama cha CHAUMA, Hashim Rungwe, Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum
Mwalimu na Kituo cha Sheria na Haki za binadamu, (LHRC) .
"Mahakama hii ina
'declare' kuwa sheria ya vyama vya siasa inakiuka vifungu vya mkataba sehemu 6
d 72 ya Jumuiya ya Afrika. Jamhuri ya Tanzania inaamriwa kurekebisha sheria ya
vyama siasa iendane na mkataba," amesema Jaji Masara akisoma uamuzi huo.
Jaji Masara anasema
mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja za kisheria na
mawakili wa pande zote mahakama imezingatia kama ina mamlaka ya kusikiliza na
kuamua shauri hili na kama sheria tajwa imekiuka mkataba wa jumuiya na kama
waleta maombi wana haki ya kufungua shauri husika.
"Mahakama hii ina
mamlaka kamili ya kusikiliza shauri hili licha ya ukweli kuwa mleta maombi
namba nne, (Sharif Hamad) ametangulia mbele ya haki," amesema Jaji
Masara akisoma uamuzi huo.
Aidha amerejea kesi
mbalimbali ambazo mahakama hiyo imefanya uamuzi kwenye mashauri yanayofanana na
hili na ambayo yapo kwenye nchi wanachama. huku akiamuru kila upande kubeba gharama za kesi.
Katika shauri hilo
linalofuatiliwa na wengi waleta maombi waliwakilishwa mawakili John
Mallya, Sheki Mfinanga na Jebra Kambole huku upande wa jamhuri ukiwasilishwa na
wakili, Vivian Method.
Awali katika
shauri hilo waleta maombi waliiomba mahakama hii itamke kuwa sheria ya vyama
vya siasa nchini Tanzania ni batili na inakiuka misingi ya kidemokrasia na
mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrika mashariki, ambao kila nchi
mwanachama analazimika kufuata ikiwemo utawala wa bora na misingi ya
kidemokrasia.
" Sheria inaruhusu
Jumuiya kusitisha uanachama wa mwanachama ambaye atakiuka utawala bora au
utawala wa kidemokrasia au atakayekiuka misingi ya haki za binadamu. Ndio
msingi wa kuundwa kwa Jumuiya," amesema Jaji Masara wakati
akisoma uamuzi huo.
Jaji Masara amevitaja
vipengelea vya kisheria vinavyolalamikiwa kwenye sheria hiyo ya vyama vya
siasa kuwa ni pamoja na kifungu kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa
nchini kuingilia wakati wowote mafunzo mbalimbali na shughuli za chama cha siasa.
"Vifungu vyote hivi
vinakiuka misingi ya utawala bora, misingi ya kidemokrasia na
inakiuka mkataba wa kuanzishwa EAC. Kifungu kinachompa mamlaka
msajili ya kumsimamisha uanachama mwanachama yeyote kushiriki shughuli za
kisiasa," ameeleza Jaji Masara.
Amesema waleta maombi
wanaomba mahakama hiyo itamke kuwa sheria hiyo ni batili na mahakama hii itoe
amri kuwapa kila aina ya nafuu ya kisheria.
"Na kwamba sheria
kumpa msajili uhuru wa kuingilia mambo ya ndani ya chama cha siasa. Na kwamba
msajili sio mtu huru kwa kuwa anateuliwa na mwenyekiti wa chama cha siasa,"
amesema na kuongeza .
... Mahakama hii inaona
kuwa nchi wanachama wanapaswa kuheshimu mkataba pamoja na mkataba wa haki za
binadamu wa Afrika.Ni jukumu la nchi wanachama kuhakikisha ustawi wa
watu,kulinda demokrasi pamoja haki za binadamu.
.... Kwa kuwa mahakama
hii ina mamlaka sasa basi mahakama inasoma swala la au sheria ya vyama vya
siasa inakiuka mkataba wa EAC.Mahakama hii inaona kuwa ni lazima sheria
inayotungwa kwenye nchi wanachama izingatie haki za binadamu,ni lazima sheria
iwe wazi kwa watu wake wajue kipi kinakatazwa na kipi kinakubali.
... Ni maoni ya mahakama
hii kuwa sheria hii inampa msajili nguvu kubwa dhidi ya vyama vya siasa jambo
ambalo ni kinyume cha mkataba wa Jumuiya kifungu cha nne cha sheria ya
vyama vya siasa.Kifungu hiki kinahusu mafunzo ya makada wa vyama vya siasa,na
sheria inataka kabla ya mafunzo lazima chama cha siasa kipeleke kwa msajili
'material' yote ya kufundishia yeye msajili ndio akubali kama hayo mafunzo ni
sawa ama la
...Waleta maombi
walilalamikia hiki kifungu kwa kuwa kinatoa mamlaka makubwa ya msajili
kupangilia nini chama kifanye.Na kiongozi wa chama cha siasa atakayekiuka
sheria hii anatenda kosa la jinai na msajili atamfungia kwa muda atakaoamua
yeye msajili.
...Kifungu hiki
kinakiuka haki ya kujieleza na haki ya kukutana kinyume cha mkataba wa
Jumuiya ya Aftika Mashariki.Kifungu hiki kinakiuka misingi ya Kidemokrasia na
utawala bora kinyume cha mkataba wa Jumuiya kwa nchi wanachama
Jaji Masara amesema kwa upande wake mjibu maombi ambaye ni mawakili wa serikali amejibu kuwa sheria hiyo haikusudii kukiuka mikataba ya kimataifa hivyo akaomba mahakama huyo itupilie mbali ombi hili.
Amedai kuwa kifungu hicho kinalenga kufanya serikali itambue,ijue kila tukio linalofanywa na vyama vya siasa.


0 Comments:
Post a Comment