MAHAKAMA KUTOA UAMUZI MDOGO KESI YA SABAYA

 



YAMEIBUKA mabishano makali ya kisheria kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya mawakili wa utetezi kuweka pingamizi mahakama isipokee vielelezo vitatu vya upande wa jamhuri kwa madai kuwa vina mapungufu kisheria.

 

Pingamizi hilo liliibuliwa jana na wakili wa Utetezi, Moses Mahuna mbele ya hakimu ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda, wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha anayesikiliza shauri hilo namba 27/2021.

 

 Pingamizi hilo liliibuliwa wakati wakili wa serikali mwandamizi, Tarsila Gervas akiomuongoza shahidi wa tisa, Mary Mayoka Kimasa(40) ambaye ni Meneja Benki ya CRDB tawi la Kwa Mromboo kuiomba mahakama kuivipokee vielelezo hivyo.

 

Vielelezo hivyo ni pamoja na nyaraka tatu ikiwemo taarifa ya akaunti (bank statement), karatasi ya kuweka na kutoa fedha kwenye akaunti, (bank slip) na kivuli cha kitambulisho cha udereva.

 

Wakikli mahuna alidai mahakamani hapo kuwa banki statement ni nakala kutoka kwenye mfumo wa benki ambapo mfumo wa benki ndiyo halisi hivyo hiyo ililetwa mahakamani ni nakala.

 

Alidai kuwa  sheria inataka nakala ifuate utaratibu wa kupokelewa  kwa nakala chini ya kifungu cha sheria namba 78 na 78 nakala hiyo inataka ushahidi huo upokelewe chini ya sheria ya miamala ya kielekroniki  chini ya kifungu cha 64 cha sheria ya ushahidi.

 

 

 

Mahuna aliendelea kudai kuwa pia sheria inataka inataka nyaraka hiyo itimize matakwa ya kifungu cha 18 cha sheria ya miamala ya kuelektroni ili vielelezo viwili, Bank statement na bank slip viweze kupokelewa mahakama pawepo na ushahidi kuwa nyaraka hiyo ni halisi na kuwe na hati inayoonyesha kuwa wakati vilipotolewa mifumo ya benki ilikuwa inafanya kazi sawasawa.

 

Akiwasilisha hoja za kupinga kivuli cha leseni ya udereva kupokelewa mahakamani hapo wakili huyo alidai kuwa inaonekana ilithibitishwa kuwa nyaraka halisi na mtu wa benki ambaye hana sifa kisheria kufanya hivyo.

 

Wakijibu hoja hizo Wakili Serikali mwandamizi, Tarsila alipinga hoja hizo za wakili Mahuna zilizoungwa mkono na mawakili wote wa utetezi kwa kile alichoieleza mahakama kuw hawakujielekeza vizuri kwenye sheria ya kielektroniki.

 

Alidai kuwa sheria hiyo ianaelekeza nayaraka za zilizotolewa kwenye mfumo wa kielektroniki itapokelewa kama matakwa mengine ya kisheria yamefuata jambo alilodai kuwa wao walifuata taratibu zote kama sheria inavyoelekeza.

 

Tarsila alidai kuwa maingizo ya vielelezo hivyo yaliyokuwa ni kawaida kama  yanavyofanyika na yalikuwa chinu ya uangalizi wa uangalizi wa (custody) ambaye  mwisho kabisa kwenye ushahidi wake alisema.

 

Alidai kuwa hivyo kwa sababu vielelezo hivyo viko kwenye  kumbukumbu cha vitabu vya benki hivyo akasema upande wa utetezi wanapotaka kuiaminisha mahakama kuwa kuwasilisha nyaraka ya benki inatakiwa kufuata sheria ya kielektroni si sahihi.

 

“Shutuma juu yangu za kutoa kielelezo si kweli, kwa sababu mimi nilikuwa namuongoza shahidi akiwasilishe kielelezo kiweze kupokelewa mahakamani na si vinginevyo, tunaomba mahakama maombi ya shahidi yapokelewe pamoja vielelezo vyake,” alaisisitiza wakili wa serikali mwandamizi Tarsila.

0 Comments:

Post a Comment