MAHAKAMA YAONYESHWA VIDEO BOKSI LA FEDHA LIKIBEBWA BENKI, WATU WAANGUA KICHEKO

 

Aliyekuwa Mkuu Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo akitoka mahakamani baada ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili pamoja na washitakiwa wenzake sita kuahirishwa.


MAHAKAMA imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na mawakili wa utetezi kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.


Aidha, kimeibuka kicheko mahakamani hapo wakati picha za video zikionyeshwa mahakamani hapo zilipoonyesha boksi lenye fedha likibebwa na watu wawili kutoka ndani ya benki ya CRDB tawi la kwa Mromboo.


Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda wa mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha anayesikiliza shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27/2021 ameeleza kuwa amefikia uamuzi wa kutupa pingamizi hilo baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande mbili pamoja na sheria ya ushahidi.


   



“Mahakama baada ya kuzingatia pingamizi la utetezi ilijikita kwenye tafsiri ya kisheria ya ushahidi na ‘electronic act’ imeonyesha kwamba vielelezo vinavyotakiwa kutolewa mahakamani vimekidhi matakwa ya sheria kupitia shahidi wa nane,” alisema Hakimu Kisinda.



Alisema kuwa maahakama imeona pingamizi halina msingi hivyo mahakama ikapokea  flash disk iliyohifadhi ripoti ya uchunguzi yenye  picha za video sita kama kielelezo namba tano cha upande wa Jamhuri.


 


Baada ya mahakama kutupa mapingamizi hayo wakili wa serikali mwandamizi, Felix Kwetukia alimuongoza shahidi  wa nane, Johnson Kisaka ambaye ni afisa uchunguzi wa kielektroniki kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini,(TAKUKURU)   kutoa ushahidi wake.


Wakati akiendelea kutoa ushahidi huo kupitia projector iliyofungwa mahakamani hapo, shahidi huyo alionyesha video ya inayoonyesha eneo la ukumbi wa  benki ya CRDB tawi la kwa Mromboo  wakati mtu aliyevaa koti refu la bluu na mtu aliyevaa tisheti nyeupe yenye mistari meusi na kofia nyeusi wakibeba boksi lenye fedha jambo lililofanya watu wote mahakamani hapo kuangua kicheko.



Awali mahakamani ikafungwa projector ikaungwanishwa kwenye kompyuta mpakato kisha kupitia wa upande wa kulia wa mahakama picha ikawa inaonekana ambapo ili zionekane vizuri mlango wa kuingilia mahakamani na madirisha mawili yalifungwa mapazia.


sehemu ya  Maswali na majibu  shahidi akiongozwa na wakili wa serikali mwanadamizi, Kwetukia


Wakili: page ya nne link ya kwanza iachie tuone mpaka mwisho

Shahidi:aliweka video inayoonyesha eneo la mbele ya benki (main Entrance) . Anaonekana mtu aliyevaa kaunda suti ya blue akishuka kwenye gari la bluu na mwingine kavaa koti refu (overall coat)  la blue mwenye kaunda suti ya bluu akazinguka nyuma ya gari akafungua mlango kisha akaufunga huku akiendelea kuongea kwa simu camera inasoma 01/20/2021 saa 16: 10 mpaka 16:36

Wakili: Twende kwenye chanel 12 

Shahidi:Anaweka video  inaonyesha ndani ya benki kuanzia saa 16:09 anaonekana mtu mwenye koti refu (overroll) aliingia benki benki akisindikizwa na yule liyevaa kaunda suti ya bluu baadye anaingia mtu aliyevaa tshirt nyeupe yenye mistari meusi na kofia nyeusi wote wawili wanakuwa karibu na na aliyevaa koti la bluu.

Wakili:weka inayofuata 

Shahidi: anaweka video inaonyesha ndani ya ukumbi wa benki  kunzia saa16:17 ambapo anaonekana mtu aliyevaa  overall ya bluu anafika kwenye dirisha la kuweka na kutoa  fedha kisha anaacha karatasi anaenda kwenye chumba upande wa kulia kijana aliyevalia  tisheti nyeupe na mistari meusi na kofia nyeusi anasimama kwenye mlango wa kuingia kwenye hicho chumba. Mara kadhaa anaonekana kuongea na watu waliovalia kama wafanyakazi wa benki lakini anaendelea kubaki. Anaonekana mtu aliyevalia nguo kama mfamyakazi wa benki wa kike akimsemesha kisha mwenye overall anatoka hapo mlangoni wanaongea kidogo halafu mfanyakazi wa kike wa benki anaondoka. Mtu mwenye koti la overall anarudi ndani na aliyevalia  tisheti nyeupe na mistari meusi akaendelea kusimama mlangoni. Akatoka 16:36 kisha akarejea tena ndani ya chumba hicho akatoka na 16:39 akaenda kwenye dirisha la kuchukulia fedha kisha akarudi kukaa kwenye viti vya wateja. Kijana mwenye tisheti nyeupe na mistari meusi akamfuata akakaa pembeni yake 16:48 mtu anayeonekana kuwa mfanyakazi wa benki anamuinamia kumsemesha kisha anaondoka.

Saa 16:50 anasimama kuelekea kwenye dirisha la kuchukulia fedha na mtu aliyevalia  tisheti ya anamfuata.

Saa 16:53 mtu aliyevalia koti (overall) la bluu anarudi kukaa kwa kiti cha wateja mtu aliyevalia  tshirt nyeupe mistari meusi anaendelea kusimama 16:57 anaenda dirisha la kuchukulia fedha na mtu aliyevalia  tisheti nyeupe mistari meusi anasimama nyuma yake.

Saa 16:58 mtu anayeoneka aliyevaa  kama mfanyakazi wa benki anampaka mtu aliyevaa koti la bluu kitu kama karatasi kubwa nyeupe iliyokunjwa anaiweka juu ya meza ndogo kwenye dirisha la kuweka na kutoa fedha.


aa 17:01 fedha zinatolewa ndani zikiwa zimebebwa kwenyew kiti cha magurudumu na mtu kama muhudumu wa benki akawa anaziweka kwenye boku  huku wawili hao aliyevaa koti la Overall bluu na aliyevaa tisheti nyeupe yenye mistari meusi  wakihakiki wakazibeba kwa pamoja. Baada ya hapo aliyevaa Overall akainama kubeba boksi la fedha na mwenye Tisheti nyeupe yenye mistari meusi naye akainama hivyo wakalibeba kwa pamoja .

Watu waliokuwa mahakamani wakacheka kwa sauti


Walipofika karibu na mlango wa kutoka nje ya benki  aliyevaa tisheti  akamuachia mwenye koti la bluu akabeba fedha hizo peke yake. 


 

Wakili: rudi kwenye ile chanel one clip ya pili


Shahidi: Akaweka video inaonyesha eneola nje ya benki kuanzia  muda saa 16:39 ambapo ilipofika saa 17:03 anaoneka  mtu mwenye koti la bluu akitoka kwenye lango la benki akiwa kabeba boksi lenye fedha  akifuatiwa kwa hyuma na mtu mwenye tisheti nyeupe yenye mistari meusi  kisha anaweka boksi lenye fedha chini pembeni ya gari anafungua mlango wa  mbele wa abiria naziweka kwenye kiti cha mbele  aha abiria anafunga mlango. Anazunguka  upande wa dereva anapanda na yule mwenye tisheti nyeupe na mistari meusi akapanda kwa mlango wa nyuma upande wa dereva gari ikaondoka.

Shahidi: akaweka video ya  nne inayoonyesha  eneo ndani ya kichumba cha kuweka na kupokea fedha ambapo anaonekana muhudumu wa benki akiwahumia wateja. Kwa nje anaonekama mtu aliyevaa koti la bluu  akifika na kukabidhi karatasi ya benki kwa mtu anayeonekana kama muhudumu wa benki. Wanaonekana kama wanaongea  kisha muhudumu anashika fedha kisha anaenda kichumba cha mhudumu wa dirisha la pili halafu anarejea anamsemesha tena mtu mwenye koti la bluu  anaondoka na mtu anayeonekama kama muhudumu wa benki anaendelea kuwahudumia wateja wengine.

Wakili: Onyesha Clip ya tano

Shahidi:Video  ya tano bado inaonyesha ndani ya dirisha la mhudumu wa benki ambapo anaonekana kukusanya mabunda ya fedha yanavyohesabiwa kisha anapeleka boksi tupu analiweka juu ya meza ya dirisha la kuweka na kutoa fedha kwa nje kisha anarudi ndani uanachukua mabunda ya fedha na kuanza kuyapanga ndani ya boksi.  

Wakili:kuna vitu umevitoa mahakamani tofauti na taarifa hii?


Shauri hilo linaendelea Novemba 2, 2021


0 Comments:

Post a Comment