Thursday, September 23, 2021

MBOWE ATAJWA KESI YA SABAYA

 

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Olw Sabaya na washitakiwa wenzake leo wakitoka kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha

MKURUGENZI Msaidizi anayesimamia utawala Wizara ya Fedha na Mipango, Renatus Msangira, (45) ameieleza mahakama kuwa akiwa msaidizi wa Katibu Tawala mkoani Kilimanjaro hakuwahi kuona maombi ya maandishi ya aliyekuwa mkuu wa wilaha ya Hai, Lengai ole Sabaya ya kwenda kufa ya kazi nje ya wilaya na mkoa wake.



Aidha amesema kuwa amesikia kesi ya  Mwenyekiti wa Taifa wa  Chama Cha Demokrasia  na Maendeleo, (CHADEMA), Freeman Mbowe lakini hafahamu mashitaka ya uhujumu uchumi na ugaidi yanayomkabili.

Pia ameeleza kuwa dereva alikuwa hakumbuki jina la dereva aliyekuwa anamuendesha Sabaya wakati akiwa DC Hai ila anakumbuka aliazimwa kutoka Jeshi la Wananchi.

Msangira meyasema hayo leo Septemba 23, 2021 mbele ya hakimu mkazi, Patricia Kisinda wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha wakati akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa serikali mwandamizi, Felix Kwetukia na akihojiwa na wakili wa utetezi Silvester 


Sehemu ya mahojiano hayo ya Msangira ambaye i shahidi wa kwanza upande wa jamhuri akihojiwa na wakili wa utetezi Silvester Kahunduka 

Wakili: Tueleze ukiwa katibu tawala msaidizi kitengo cha rasilimali watu na utawala dereva wa Mkuu wa wilaya ya Hai alikuwa anaitwa nani 
Shahidi: Sikumbuki  
Wakili: Una mfahamu aliajiriwa lini?
Shahidi: Kwa kumbukumbu zangu yule dereva aliazimwa kwenye jeshi la wananchi 
Wakili: unafahamu kuna kesi ua uhujumu uchumi na ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake
Shahidi: Nafahamu lakini siwezi kujua kama anakabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi na ugaidi.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa serikali mwandamizi Felix Kwetukia shahidi huyo wa kwanza wa jamhuri aliieleza mahakama  kama sehemu ya mahojiano yao kama ifuatavyo

 Wakili: Wewe kama mkuu rasilimali watu mkoa siku ya tarehe 22 Januari,2021 aliyekuwa mkuu wa wilaya ya hai Lengai ole Sabaya alipata ruhusa kwenda eneo gani katika kutekeleza majumu yake
Shahidi; Sijawahi kukutana na barua ya kuomba ruhusa kwa tarehe hiyo
Wakili: wewe unaongeleaje utaratibu wa Mkuu wa wilaya kutoka nje ya wilaya yake na mkoa wake bila kibali?
Shahidi: Kama nilivyosema, kutoka nje ya kazi bila ruhusa ya mkuu wa kituo cha kazi ni kukiuka utaratibu.
Wakili; Wewe kama katibu tawala msaidizi ungejua Mkuu wa wilaya ya Hai amepata ruhusa ya kutoka nje ya wilaya yake na mkoa wake?
Shahidi; Inaeleweka ili utoke nje ya kituo cha kazi lazima uwe na ruhusa ya maandishi na mkuu wa wilaya Hai alipaswa kuomba ruhusa kwa maandishi.
Wakili; Wewe ungefahamuje kuwa mkuu wa wilaya ya Hai ameomba ruhusa?
Shahidi: Mheshimiwa hakimu, ningeletewa barua na bosi wangu (RAS)  kuonyesha Mkuu wa wilaya ya Hai yumo nje ya kituo chake cha kazi.
Wakili; Ulisema pia unasimamia vitendea kazi ikiwemo magari  tueleze utaratibu wa kutoka na gari sehemu moja kwenda nyingine
Shahidi: Kama  unaomba  ruhusa ya kwenda na gari inapaswa kuandikwa kimaandishi ili kuwezesha kujua gari fulani la mkoa liko sehemu fulani, anatekeleza , majukumu fualani kulingana na barua ya mwaliko.
Wakili: Bwana Renatus unafahamu nini juu gari ya mkuu wa wilaya hai kwa kipindi hicho kufanya safari kutoka hai kwenda Arusha.
Wakili wa utetezi Moses Mahuna akasimama kupinga swali hilo lisijibiwe kwani linamuelekeza shahidi cha kusema ambapo Hakimu Kisinda akamuelekwza Qakili wa serikali Kwetukia kuliweka vizuri swali lake 

Wakili: Nilikuuliza pale mwamzo suala la gari, ni ombi gani lilifikishwa mbele yake kuomba gari kutoka nje ya wilaya ya Hai
Shahidi: Sikuwahi kuona ombi kama hilo.
Wakili: Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya wewe unamfahamu vipi?
Shahidi: Alikuwa ni mmoja wa mtumishi ambaye tunamlipa mshahara mkoa wa Kilimanjaro kwa vote 75 
Wakili: Katika utendaji wake wa kila siku mara nyingi alikuwa anaambatana na mtu gani?
Shahidi: Kwa siku ambazo tulikuwa tunakutana naye mmoja wa watumishi ni dereva wake na kuna watu alikuwa anaambatana nao. Derava ambaye sisi tulikuwa tunamtambua ambaye alikuwa nalipwa stahili za serikali na wengine alikuwa anaambatana nao hatukuwafahamu
Mahuna mh hakimu wakili wa serikali.
Wakili; Katika ziara ambazo mlikuwa mkikutana ni watu wangapi walikuwa wanakuwa kwenye msafara wa Sabaya.
Shahidi: Mheshimiwa kiukweli nilikuwa namuona mheshimiwa Sabaya akiwa na kijana mmoja ambaye walikuwa wanafanana fanana na sikutaka kumtambua kwa kuwa si jukumu langu na wengine 
Wakili: Umeongea kwa kirefu kuhusu Lengai ole Sabaya akiletwa hapa unaweza kumfahamuaje?
Shahidi: Akiletwa hapa namtambua kwa sababu alikuwa liongozi wa serikali labda awe amebadilika sana
Wakili: Na huyo kijana aliyekuwa akifuatana naye aliletwa utamtambuaje?
Shahidi; Alikuwa smart alikuwa anamyoo fulani wa nywele wa kupendezesha anapiga koti kama bosi wake (Anatabasamu)
Wakili; Embu isaidie mahakama kwa kuwagusa bega
Shahidi: Mheshimiwa kwa ruhusa yako naomba (washitakiwa) wavue barakoa
Hakimu: Sogea pale 
Shahidi; Komredi  (shahidi ananyoosha kidole huku akimtazama Sabaya)
Mahakama kicheko
Wakili; Mshike bega
Shahidi akaomba washtakiwa wengine wavue barakoa ili awatambue 
Shahidi: Huyu hapa huku akimshika bega  mshitakiwa wa tano Sylvester Nyegu.
liyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Olw Sabaya na washitakiwa wenzake leo wakitoka kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha



Washitakiwa wengine kwenye shauri hilo ni pamoja na Enock Mnkeni, (41) maarufu  Dikdik, Watson Mwahomange, (27) maarufu Mamimungu, John Aweyo, maarufu  Mike One, Silvester  Nyengu, (26) maarufu Kicheche, Jackson Macha, (29) na Nathan Msuya, (31).


Katika shauri hilo linalofuatiliwa na wananchi wengi washitakiwa wanakabiliwa na makosa matano ya ambapo shitaka la kwanza na la tano linawahusu washitakiwa wote saba ambapo wanashitakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji wa fedha huku shitaka la pili, la tatu na la nne yakimkabili Sabaya peke yake ambayo ni mashitaka ya rushwa  na matumizi mabaya ya ofisi.

Shauri hilo linaendelea kesho Septemba 24, 2021 washitakiwa wamerejeshwa mahabusu kwenye gereza la mkoa la Kisongo.

No comments:

Post a Comment