Wednesday, September 22, 2021

PINGOS YAWALETA PAMOJA WADAU WA MAPAMBANO YA UKATILI WA JINSIA

 

 

 

SHIRIKA la Mtandao wa mashirika ya Wafugaji, Wawindaji na Waokota Matunda nchini, (PINGOS), limewakutanisha Maafisa maendeleo ya jamii, wakuu wa dawati ya jinsia ya polisi, maafisa ustawi wa jamii, mshirika yasiyo ya Kiserikali, (NGO) wafugaji na wakulima kutoka mikoa ya  Arusha, Kilimanjaro, Tanga, na Manyara.

 

Washiriki hao zaidi ya 30 wamekutana kwa siku mbili Wilayani Arumeru kwa lengo la kuweza kujadilia namna bora ya kushirikishana maswala ya jinsia sanjari na kuhakikisha kuna ushiriki mkubwa kwa kinamama katika swala la uongozi na utawala Bora.

 

 

 

Mkurugenzi wa shirika PINGOS, Edward Porokwa akiongea na washiriki hao wakati akifungua mafunzo hayo amesema anaamini mafunzo hayo yatasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijinsia kwenye jamii hizo.

 

 

 

Mafunzo hayo yamewakutanisha washiriki zaidi ya  30 kutoka jamii za wafugaji kwenye  wilaya za Ngorongoro, Longido, mkoani Arusha na Hanang’ na Simanjiro mkoani Simanjiro na Handeni Mkoani Tanga.

 

 

 

Amesema kuwa unyanyasaji wa kijinsia imekuwa ukichangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili kwenye jamii huku wanawake wakiwa hawapewi nafasi za uongozi kwenye jamii.

 

 

Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Simanjiro, Asia Ngalisoni amesema kuwa vitendo vya ukatili kwenye jamii ya wafugaji vimekuwa vikipungua kutokana na elimu shirikishi ambayo imekuwa ikitolewa na serikali kwa kushirikiana na asasi za kiraia.

 

Ameelezea nafasi ya mwanamke ya uongozi kwenye jamii ambapo amesema kuwa mfumo dume imekuwa changamoto inayowanyima wanawake kuwania nafasi za uongozi

 

 

Porokwa amesema kuwa wamegundua  kuwa kuna mfumo dume kwa jamiii kutokana na iila na desturi mbaya ndani ya jamii ambapo kinamama  wamekuwa wakinyanyaswa huku  wanaume wakipendelewa sana hivyo akawataka washiriki hao kuangalia ni namna gani ya kuwatia moyo kinamama ili waweze kuwa imara ndani ya jamii

 

Amesema kuwa changamoto wanazokutana ni pamoja na uweke uwezo  mdogo wa kinamama  wa namna gani ya kukabiliana na matatizo ya ukatili ya kijinsia, kukosa ushirikiano kwa wanaume ,na mwamko  mdogo wa kinamama kushiriki Semina mbalimbali 

 

Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii kutoka Wilaya ya Longido Atuganile Chisunga amesema kuwa, matukio ya unyanyasaji kijinsia kwa wanawake yamekuwa machache ukinganisha na zamani kutokana na jitihada wanazozifanya za kutoa elimu na kuchukua hatua kali za kisheria 

 

Amesema kuwa, vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikifanyika kwa kinamama, na watoto kutokana na mila na desturi za wenyeji wa wilaya hiyo ambao ni Wamaasai jambo waliloamua kukabiliana nalo kwa kuweka nguvu kazi ya kutoa elimu hasa kuwahamasisha wazazi kuwapeleka watoto wa kike shule. 

 

“Eneo la Namanga limekuwa na changamoto ya  malezi na makuzi kwa watoto kwani wanalelewa malezi ya kunyanyaswa kwa kuwatumikisha watoto wao kazi ikiwa ni pamoja na swala la vitendo vya kulawiti. Lakini kwa sasa hali imebadilika kwa kiasi kikubwa baada ya ofisi yangu kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali kumua kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa wanajamii kuanzia ngazi ya mtaa,” anasema Chisunga. 

 

Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Simanjiro, Asia Ngalisoni amesema kwenye  wilaya hiyo  vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia  vimepungua ukilinganisha na miaka iliyopita.

 

 

“Mipango ya sera ya ulinzi na usalama kwa watoto imesaidia sana pamoja na maafisa maendeleo ya jamii kwenye ngazi zote kutokaa maofisini bali wanakwenda ndani ya jamii kupata taarifa na kuendelea kutoa elimu ya kuwalinda wanawake na watoto wa kike na ukatili wa kijinsia,” amesema Ngalisoni.

 

Hata hivyo ameiomba serikali kuongeza maafisa maendeleo ya jamii ili wawe kwenye kila kata jambo litakalosaidia kupunguza ongezeko la ukatili wa kijinsia ndani ya jamii hasa kwa kinamama na Watoto. 

 

 

No comments:

Post a Comment