BASHUNGWA AIPONGEZA AIAA KWA KULEA VIPAJI




WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amepongeza hatua ya  Chuo cha Uhasibu Arusha, (IAA) kwa  kulea na kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji vya mpira wa Kikapu, mpira wa wavu na  riadha  nchini.


Bashungwa ametoa pongezi hizo hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo amesema jambo hilo ni jitihada za kuunga mkono agizo la Rais, Samia Suluhu Hassan pamoja na jitihada za Wizara za  mkakati wa kuanzisha Shule za Michezo katika kila Mkoa kwa ngazi ya Shule za Msingi na Sekondari.



"Napenda kutoa wosia kwa vijana nchini pamoja na kupenda taaluma za  shule za msingi sekondari n vyuo taluma hizi tusisahau  vipaji vingine tulivyopewa na Mwenyezi Mungu kwasababu katika maisha hujui kipaji kipi  kitakupa ajira kwahiyo una weza kupata ajira kupitia taaluma lakini pia unaweza kupata ajira kutokana na vipaji ambavyo Mwenyezi Mungu amekupatia" amesema Bashungwa.


 Ameongeza kwa  kutoa wito kwa vijana walioko shuleni pamoja na Vyuo  kuhakikisha wanaendeleza  vipaji vyao kwa kuwa Serikali  inaunga mkono jitihada hizo na kuendelea kuweka mazingira wezeshi.

0 Comments:

Post a Comment