SIDO YAWANOA WATAALAM WA HALMASHAURI ZOTE ARUSHA KUANZISHA KONGANO


SHIRIKA la viwanda vidogo Nchini,  (SIDO),mkoani  Arusha, limetoa mafunzo kwa halmashauri zote mkoani hapa juu ya namna ya  kuanzisha Kongano za viwanda  ili kuongeza ajira na kukuza mnyororo wa thamani kwa bidhaa na mazao ya wakulima.



Meneja wa SIDO mkoani hapa, Nina Nchimbi amesema  kuwa mafunzo hayo yanalenga kuhamasisha halmashauri hizo ziweze kuanzisha Kongano za viwanda na hivyo kuzalisha ajira zipatazo milioni 8 kwa Watanzania kupitia mpango huo wa kuongeza thamani ya mazao.

Mafunzo hayo yamefanyika Aprili 30, 2021 na  kuwahusisha maafisa , biashara, kilimo, ushirika na  mipango kutoka halmashauri zote Mkoa wa Arusha.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika la kimataifa la maendeleo ya Japan, (JICA), Sido na ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha.



Nchimbo amesema mpango kama huo umeonyesha mafanikio makubwa kwenye nchi za Sweden, Vietnam na Australia.


Amesema kwa hapa nchini Kongano zilizoanzishwa na kutoa mafanikio makubwa kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Mtiko Singida, Mpunga Ubaruku mbeya, Mchikichi Kigoma, Mchele Mbeya  pamoja na kuziboresha Kongano bubu ili zilete mafanikio .

Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, (RAS), Hargeney  Chitukulo amezitaka halmashauri zote mkoani hapa kuwa tayari kutenga maeneo ya kuanzisha Kongano hizo za viwanda ili bidhaa zitakazozalishwa ziweze kupata soko kwa urahisi na kuboresha bidhaa za uzalishaji.

Chitukulo ambaye ni RAS Msaidizi ,huduma za kiuchumi na uzalishaji Mali mkaonk hapa amesema uanzishaji wa Kongano hizo utasaidia sana kukuza biashara ya wananchi hivyo kuinua uchumi wa mkoa  na Taifa.



Mmoja ya washiriki wa mafunzo hayo, afisa biashara wa halmashauri ya jiji la Arusha, Privanus Katinhila 
amesema uanzishaji wa Kongano za viwanda utakwenda kujibu Kero za wafanyabiashara kwa kuwaunganisha pamoja katika uanzishaji wa viwanda.

"Sekta binafsi kupitia Kongano za viwanda zinaenda kuwa msaada mkubwa kwa serikali kwa  kutengeneza ajira kwa vijana," alisema Katinhila.








0 Comments:

Post a Comment