August 20 usiku taarifa zilidai kuugua kwa Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya wakati akiwa rumande baada ya kukamatwa na Polisi Tarime ambapo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya Tarime.
VOA TV Imempata Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Hippolite Tarimo ambaye amesema hali ya Mbunge huyo inaendelea vizuri na tayari ameandikiwa rufaa ya kwenda Hospital kubwa kwa uchunguzi zaidi.
Ester Bulaya aliugua akiwa rumande baada ya kushikiliwa na Polisi kufuatia kumkamata akiwa Hotelini Tarime August 19, 2017.
No comments:
Post a Comment