Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua rasmi Meli Mbili kubwa za Mizigo ambazo zimetengenezwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 11.7. Meli hizo za mizigo zimekamilika, na meli nyingine ya Abiria iko katika hatua ya mwisho ambapo kwa pamoja meli hizo zinatarajiwa kuimarisha usafiri na usafirishaji ndani ya ziwa nyasa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepongeza hatua za kukamilika kwa meli hizo mbili za mizigo, na kutoa pongezi kwa mkandarasi Songolo Marine ambaye amekuwa mtanzania wa kwanza kuunda meli, baada ya muda mrefu Taifa kutegemea meli kutoka Nje ya Nchi.
Kaimu mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini TPA-Karim Mataka amemwambia waziri mkuu kuwa ujenzi wa Meli hizo ulianza miaka miwili iliyopita.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya ambapo ziara yake ameianzia wilayani Kyela na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ambapo amewaagiza madiwani kuacha migogoro na tofauti zao, badala yake wawatumikie wananchi. Chanzo Tbc 1 .
No comments:
Post a Comment