Friday, June 2, 2017

UPDATES: MAKALA; Nimekuletea yafuatayo kufuatia kutolewa bungeni Mh. John Mnyika , Sababu, alivyodhalilishwa na yaliyojiri bungeni




  1. MNYIKA ATOLEWA BUNGENI KWA AMRI YA SPIKA


Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ametolewa nje ya Bunge leo Ijumaa kwa agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Licha ya adhabu hiyo, amemzuia kutohudhuria vikao vya Bunge kwa siku saba kuanzia leo.
Mnyika ametolewa baada ya mmoja wa wabunge kusema 'Mnyika mwizi' akimhusisha na wizi wa madini, hoja inayochangiwa na wengi kwenye mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini unaoendelea.

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ametolewa nje ya Bunge leo Ijumaa kwa agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Licha ya adhabu hiyo, amemzuia kutohudhuria vikao vya Bunge kwa siku saba kuanzia leo.
Mnyika ametolewa baada ya mmoja wa wabunge kusema 'Mnyika mwizi' akimhusisha na wizi wa madini, hoja inayochangiwa na wengi kwenye mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini unaoendelea.

Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua kwa mbunge aliyemuita mwizi lakini Spika alisema hajui hilo na halojaingia kwenye ansadi 

Mnyika alisema mambo hayaendi hivyo,katika majibizano Spika aliamuru kutolewa nje na walizi wa bunge.

Mnyika alikua akitolea taarifa ya mbunge wa Livingstone Lusinde aliyekua akisema wapinzani wanatetea wezi.



Kilichojiri hasa Mnyika kutolewa bungeni kwa amri ya Spika

Chanzo kilikuwa Lusinde kunukuu hotuba ya Mnyika mahali palipoandikwa "Rais makini kabla ya kufikiria makinikia angefikiria madini yanayochimbwa na kuchenjuliwa kwa ukamilifu hapa nchini lakini nchi haipati mapato yanayostahili".

Ndipo Mbunge Lusinde wakati akichangia,  akasema Mnyika amesema Rais sio makini na kwamba upinzani ndiyo sio makini na akasema upinzani unatetea wezi. 

Mnyika akasimama kuomba utaratibu kwamba sio kweli kuwa upinzani wanatetea wezi na kwamba kama ni wizi umekuwa ukifanyika chini ya Serikali ya CCM na kwamba hata sasa pamoja na mchanga kuzuiwa, madini ikiwemo dhahabu yanaendelea kusafirishwa na kama ni wizi bado unaendelea chini ya Serikali ya CCM. 

Wakati Mnyika anaendelea, mbunge mwingine wa CCM akawasha kipaza sauti na kusema "Mnyika mwizi". Mnyika akamuomba Spika amwelekeze mbunge huyo ama athibitishe au afute kauli. Spika akasema kuwa hajasikia. Mnyika akataka basi aagize kauli hiyo ifutwe, lakini badala yake Spika akaagiza Mnyika atoke bungeni. Wakati Mnyika anatoka bungeni, Spika akaagiza askari wamtoe nje.




Endelea kubaki nami ikiwa ni pamoja na kwenye Mitandao ya kijamii Facebook ,Twitter, Instagram,  kote kwa jina la Habari Tanzania Grace Macha  bila kusahau kutazama Latest Videos zote katika V.O.A TV YouTube

No comments:

Post a Comment