Kampuni ya Takata yawasilisha hati ya kuomba isifilisiwe


Kampuni iliyokumbwa na kashfa ya utengenezaji wa mifuko hewa ya kujilinda itokeapo ajali ya Takata, imewasilisha hati ya kuomba isifilisiwe kwenye mahakama ya Tokyo kufuatia hatua ya kurudisha tena kiwandani mifuko hewa yenye hitilafu iliyotengenezwa na kampuni hiyo.

Viongozi wakuu wa kampuni hiyo ya Takata walifanya maamuzi hayo kwenye mkutano wao wa bodi uliofanyika asubuhi ya leo Jumatatu.
Madeni ya kampuni hiyo yamezidi yeni trilioni moja au takribani dola bilioni tisa za Kimarekani. 

Madeni hayo yanajumuisha gharama za kurejesha mifuko hewa yenye hitilafu ambazo zilibebwa na makampuni ya utengenezaji wa magari. Kushindwa kwa uendeshaji wa kampuni kutokana na deni la zaidi ya yeni trilioni moja ni anguko kubwa kuwahi kutokea kwa wazalishaji wa Kijapani.

Soko la hisa la Tokyo, TSE limeamua kuwa mwezi ujao litaondoa hisa za kampuni hiyo iliyo kwenye matatizo. Soko hilo la hisa lilitangaza uamuzi huo leo Jumatatu baada ya mahakama ya Tokyo kupokea hati ya kampuni ya Takata ya kuomba isifilisiwe. Hisa za kampuni hiyo zinaweza kuuzwa kwenye soko hilo mpaka tarehe 26 Julai ambayo itakuwa siku moja kabla ya tarehe iliyopangwa ya kuziondoa sokoni hisa hizo.

0 Comments:

Post a Comment