Mkuu wa zamani wa Polisi ya Federali ya Marekani (FBI) amesema kuwa Rais Donald Trump wa nchi hiyo ni mrongo na kidhabi.
James Comey ambaye alikuwa akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Upelelezi ya Baraza la Seneti la Marekani inayochunguza faili la tuhuma kwamba, Russia iliingilia uchaguzi wa rais wa nchi hiyo amesema kuwa, hadi sasa hakubaliani na hatua ya Trump ya kumuachisha kazi na kwamba Rais huyo wa Marekani alitoa tuhuma zisizo sahihi dhidi yake na FBI baada ya hatua hiyo.

Mwezi uliopita Rais Donald Trump wa Marekani alimtimua Mkuu wa Idara ya Polisi ya Federali ya nchi hiyo (FBI), James Comey kwa tuhuma kwamba, hakutekeleza vyema majukumu yake kuhusiana na kashfa iliyozua makelele mengi ya bauapepe za Hillary Clinton ambaye alichuana na Trump katika kinyanganyiro cha uchaguzi wa rais wa mwaka jana.
Hata hivyo Wademocrats wanasema, sababu ya kufukuzwa kazi James Comey ni sisitizo lake la kudumishwa uchunguzi kuhusu ushirikiano wa siri baina ya jamaa wa karibu na Donald Trump na Russia.
No comments:
Post a Comment