Monday, May 29, 2017

WASIWASI ZAIDI: Korea Kaskazini yarusha Kombora lingine . Kaa nami ili usipitwe na updates zote Mara tu zinapotokea


Wizara ya Ulinzi nchini Japani imesema Korea Kaskazini imerusha kombora leo Jumatatu asubuhi. Maafisa wa serikali ya Japani, wanaamini kuwa kombora hilo limeanguka kwenye ukanda maalum wa kiuchumi wa Japani, katika Bahari ya Japani. 

Waziri Mkuu wa Japani, Shinzo Abe, amesema Japani itafanya kazi na Marekani kuzuia vitendo vya kichokozi kutoka Korea Kaskazini, na kuongeza kuwa itafanya kazi kwa karibu na jumuia ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Korea Kusini ili kudumisha viwango vya juu vya usalama. 

Jeshi la Korea Kusini limesema kombora hilo liliruka takribani kilomita 450 kabla ya kuanguka baharini. Lilisema kombora hilo lilirushwa kutoka pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini, na inaminika kuwa ni kombora la Skadi. 

Katibu mkuu wa Baraza la Mawaziri la Japani, Yoshihida Suga, amesema hakuna meli au ndege zilizopata madhara katika eneo hilo. Ameongeza kuwa, urushwaji wa kombora hilo unakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuwa Japani inapinga vikali urushaji huo wa kombora uliofanywa na Korea Kaskazini . 

Kwa mwaka huu hadi Mei 21, Korea Kaskazini imerusha makombora 11.

No comments:

Post a Comment