Thursday, May 18, 2017

VIDEO UPDATES: Ni baada ya tukio la kukamatwa waandishi wa Habari na viongozi wa dini Arusha

Viongozi mbalimbali wa dini na wamiliki wa shule mbalimbali wakiwa katika ibada maalum ya kuwa kuwapa pole wafiwa wa msiba ulioikumba taifa wa Lucky Vicent Arusha.

Ilikuwa mapema Ibada maalum ya kuwapa pole wazazi walioondokewa na watoto wao katika ajali iliyotokea hivi karibuni ya gari la shule ya Lucky Vicent kupata ajali na kupelekea vifo vya wanafunzi 32 Dereva na waalimu kadhaa waliokuwemo katim gari hill.

Ibada hiyo ilikuwa na leongo la kuwapa pole wazazi waliofiwa na watoto wao katika ajali hiyo , pole hizo ziliambatana na rambi rambi kutoka kwa shirikisho la wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini Tanzania.TAMONGSCO)

Katika hafla hiyo shirikisho hill liliwamislishwa na katibu wake kanda ga kaskazini Bw. Leornad Mao.

Wakati ufunguzi wa shuguli hiyo ukiendelea kulitokea hali ya sintofahamu ambapo aliingia OCD Damasi Masawe nakuwataka watu wote wawe chini ya ulinzi kwa madai kuwa shughuli hiyo IPO kinyume na sheria ya nchi kwamba mikusanyiko isiyo pewa kibali maalum na Jeshi la polisi havitakiwi.

OCD hatimaye aliamuru viongozi wore pamoja na waandishi wa Habari watoke nje na kuandikwa majina na kupelekwa kituo kikuu cha polisi (Central) .

Safari kuelekea Central ikaanza ambapo kwa ujumla walikuwa akishikiliwa Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro , viongozi wa dini na waandishi wa Habari.

Waandishi wa Habari walikaa central kwa muda wa SAA mbili na hatimaye kuachiliwa huru huku viongozi wa dini na Meya wakiendelea kuhojiwa.

Kwenye video hapa anaeleza Mmoja wa waandishi waliokamatwa Arusha 

Ni tukio lililotokea ambalo liligusa nyoyo za watu , ikumbukwe wakati akiingia Afisa huyo wa kitengo cha upelelezi wa polisi kulikuwa kuendelea ibada ya ufunguzi wa ibada hiyo hivyo watu walikuwa wakiomba.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha katika mahojiano na waandishi wa Habari alisema kilichofanya watu kukamatwa ni kutokana na Jeshi hilo la polisi kutokuwa na taarifa juu ya uwepo wa ibada na kusanyiko hilo.

"Tulisikia kuna mkutano Lucky Vicent na haukuwa na kibali ikabidi tuchukue hatua,  tulikuwa tunataka kujua usahihi wa kusanyiko hilo. "

"Uchunguzi wa jeshi la polisi umebaini kuwa lengo la kusanyiko hilo ilikuwa umoja wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi kukabidhi rambi rambi "

Kubusu Waandishi waliokamatwa Kamanda huyo anasema "waandishi walikamatwa kimakosa"

No comments:

Post a Comment