Wednesday, May 31, 2017

UPDATES: MAREKANI IMEFANIKIWA KUDUNGUA MAKOMBORA YA BARA HADI BARA


Imekuwa ni Korea Kaskazini kwenye headlines kuhusu kufanya majaribio ya makombora ya masafa ya kati na Masada Marefu ambapo hadi kufikia sasa Korea Kaskazini imeshafanya zaidi ya Majaribio 10 huku nyingi kati hii zikilekezwa kwenye ukanda uchumi Wa bahari ya Japan na mengine kadhaa yakielekezwa angani na kuangia baharini.

Jumatatu Marekani iliaema imechoshwa na vitendo vya Mara kwa Mara vya kichokozi vinavyofanuwa na Korea Kaskazini na kwamba njia za Kidiplomasia zimeshindikana ikiwa ni pamoja na kuliwekea vikwazo Taifa hill dogo la Korea Kaskazini.

Marekani ilitangaza kwamba Leo Jumatano itafanya jaribio la kombora lake ambalo litakwenda bara moja hadi nyingine ikiwa ni pamoja na kuweka mtambo wenye uwezo Wa kudungua makombora ya nyukilia kutoka bara moja hadi lingine.

Leo nimekuaogezea taarifa ikieleza mafanikio ya Marekani katika kudungua makombora kutoka bara moja hadi lingine.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema imefanikiwa jaribio lake la kwanza la aina yake la kudungua kombora lenye uwezo wa kuvuka mabara kwa kutumia mfumo wa kudungulia makombora ulio ardhini. 

Wizara hiyo jana Jumanne ilisema kuwa kombora hilo la udunguaji lilirushwa kutokea kambi ya jeshi la anga ya Vandenberg iliyo California nchini Marekani na ilidungua mfano wa kombora lenye uwezo wa kuvuka mabara lililorushwa kutoka kwenye eneo lililoko visiwa vya Marshall. 

Wizara hiyo imesema jeshi la nchi hiyo lilifuatilia kombora hilo lenye uwezo wa kuvuka mabara kwa kutumia rada aina ya "X-band" lililopokuwa linavuka Bahari ya Pasifiki. 

Wizara hiyo ya Ulinzi imesema uwezo huo wa kudungua kombora lenye uwezo wa kuvuka mabara ni mafanikio makubwa na inadhihirisha kuwa Marekani ina uwezo thabiti wa kuzuia tishio lolote dhahiri. 

Mfumo huo wa ardhini wa kudungua makombora uliwahi kufanikiwa kwenye majaribio tisa kati ya 17 yaliyowahi kufanyika kati ya mwaka 1999 na 2014. 

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo Korea Kaskazini inaendelea na mpango wake wa kuendeleza nyuklia na makombora yenye uwezo wa kuvuka mabara. 

Marekani imekuwa ikiendeleza mfumo wake wa kujilinda dhidi ya makombora wenye lengo la kulinda eneo lake la bara. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu nchi hiyo inapanga kuwa imepeleka makombora yake nane ya udunguaji kwenye jimbo lake la Alaska





Endelea kubaki nami ikiwa ni pamoja na kwenye Mitandao ya kijamii Facebook ,Twitter, Instagram,  kote kwa jina la Habari Tanzania Grace Macha  bila kusahau kutazama Latest Videos zote katika V.O.A TV YouTube.

No comments:

Post a Comment