Sunday, May 28, 2017

UPDATES: Ni Nape Tena kwenye headlines , Leo azungumzia sababu ya kuikosoa sana Serikali.


Aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Habari na Michezo Nape Nnauye na Mbunge wa Mtama (CCM) amezungumza yafuatayo baada ya fununu kuenea kuwa anaikosoa serikali kwakuwa ameondolewa kwenye uwaziri.
Hivi karibuni Tangu kuondolewa katika nafasi ya uwaziri nape ameonesha upinzani mkali dhidi ya serikali hususani anapokuwa Bungeni katika vipindi vya majibu na maswali.
Kwanza ni vizuri watu wakaelewa kwamba Wabunge kutoa mawazo na kushauri hakuna maana ya kuikosoa serikali au kumdhalilisha Rais na serikali yake bali ni wajibu wetu kama wabunge.
“Sisi kama wabunge tuna hasa wa CCM ndio zaidi tunapaswa kuishauri vizuri serikali ili utekelezaji wa Ilani utekelezeke.
“Kuna watu wanahoji kwanini sasa hivi naonekana kuishauri serikali sasa hivi nikiwa mbunge wa kawaida, Unajua ukiwa Waziri na wewe unakuwa ni sehemu ya serikali na mnashauriana katika vikao vya ndani.
“Wanaosema kwanini sasa hawajui nilikuwa nafanya nini nikiwa ndani ya serikali na hayo ni mawazo yao, Ukiwa mbunge nafasi yako ni ndani ya bunge hivyo naitumia nafasi yangu vizuri kwa mujibu wa katiba nikiwa kama Mbunge.” – Nape Nnauye.

No comments:

Post a Comment