Sunday, May 28, 2017

HIVI PUNDE: Viongozi wa G7 Wamaliza mkutano Bila mafanikio juu ya Mabadiliko ya Tabia ya nchi.


Viongozi wa kundi la nchi saba zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani, G7, wamefikia maafikiano juu ya kupambana na sera ya kulinda biashara za ndani lakini hawakuweza kukubaliana kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi. Huo ni ujumbe kwenye taarifa ya pamoja baada ya kumalizika mkutano wa siku mbili wa viongozi hao wakuu nchini Italia. 

Katika taarifa hiyo, viongozi waliidhinisha biashara huru wakiahidi kupambana na kupambana na sera ya kulinda biashara za ndani. Rais Donald Trump wa Marekani alichelewesha kutoa taarifa kama hiyo siku za nyuma. Hata hivyo viongozi wa G7 walisema walishindwa kufikia maafikiano kuhusiana na makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kuhusiana na Korea Kaskazini, viongozi hao walisema nchi hiyo ni tishio kubwa. Waliitaka Korea Kaskazini kutekeleza kwa ukamilifu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuachana na mipango ya nyuklia na makombora.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano, Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe alijikita kwenye suala la Korea Kaskazini.

Abe alinukuliwa akisema;" Suala Korea Kaskazini haliziathiri nchi za Mashariki mwa Asia pekee bali dunia nzima kwa ujumla. Tumethibitisha hili na viongozi wengine wa G7. Kinachohitajika sasa ni kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua stahiki zinazokidhi utawala wa sheria."

Pia alisisitiza juu ya jukumu muhimu kwa nchi za China na Urusi linapokuja suala la Korea Kaskazini. Abe pia alizungumzia umuhimu wa ushirikiano wa kibiashara kama Makubaliano ya Biashara Huru kwa nchi za Pasiki. 

Abe alisema, " Japani itafanya kila iwezalo kusimamia uchumi huru na wenye uwiano unaotokana na misingi ya sheria. Ninataka kuchukua jukumu ongozi kwenye suala hilo."

No comments:

Post a Comment