Tuesday, May 30, 2017

UPDATES: Kufuatia Korea Kaskazini kuendelea na Urushwaji Wa Makombora , Raia Korea Kusini wailaumu Marekani, Waandamana nchi nzima

 Raia wa Korea Kusini wamefanya maandamano makubwa katika miji tofauti ya nchi hiyo hususan Seoul, mji mkuu wa taifa hilo ambapo mbali na kutaka kusimamishwa haraka uwekaji ngao ya makombora ya Marekani, wametaka pia kuondolewa askari wa nchi hiyo katika eneo la Korea.
Maandamano hayo ya kupinga uwekaji ngao ya kisasa ya makombora ya Marekani yamefanyika ikiwa ni katika kuunga mkono sera za serikali mpya ya nchi hiyo juu ya suala hilo. Kwa mujibu wa habari kutoka Seoul, maandamano makubwa yameshuhudiwa katika maeneo ya jirani kunakojengwa ngao hiyo ya makombora ya kaunti ya Seongju iliyo kilometa 300 kutoka mji wa Seoul. Kwa mujibu wa waandamanaji hao, uwekaji ngao hiyo ya makombora, utaathiri kwa kiasi kikubwa hali ya hewa sambamba na kuisababishia hasara kubwa nchi yao katika kudhamini fedha za kuendesha ngao hiyo.


Raia wa Korea Kusini katika maandamano

Kadhalika raia wa Korea Kusini wanapinga uwekaji ngao hiyo kwa kile walichokisema kuwa ni kushadidisha uhasama baina ya nchi yao na nchi jirani ikiwemo Uchina. Kadhalika Wakorea Kusini wametaka kuondoka askari wa Marekani katika nchi hiyo na kwamba uepo wa askari hao eneo la Korea unazidi kuhatarisha usalama wa nchi yao. Kadhalika wamesisitiza kuwa, Washington inaendesha propaganda za kuonyesha Korea Kaskazini na China kuwa ni hatari, kwa lengo la kudhaminia maslahi yake katika eneo la Peninsula ya Korea. Hii sio mara ya kwanza kwa raia wa Korea Kusini kufanya maandamano kupinga siasa za Marekani dhidi ya nchi yao hususan katika suala zima la uwekaji wa ngao hiyo ya makombora. Siasa za kupenda kujitanua Marekani eneo la Peninsula ya Korea, zimefanya hali ya mambo katika eneo hilo kuwa tata zaidi siku hadi siku.

Endelea kubaki nami ikiwa ni pamoja na kwenye Mitandao ya kijamii Facebook ,Twitter, Instagram,  kote kwa jina la Habari Tanzania Grace Macha  bila kusahau kutazama Latest Videos zote katika V.O.A TV YouTube.

No comments:

Post a Comment