Tuesday, May 30, 2017

HABARI NJEMA: TANAPA imetoa ofa ya siku mbili Wananchi kutembelea hifadhi za Taifa bure.

Hii in Habari njema mtu wangu Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA imetoa of a Maalum kwa ajili ya wananchi.

Tanapa limetoa taarifa mahsusi kuwa watanzania wanaweza kuitembelea hifadhi za taifa bila malipo ikiwa ni katika jitihada za wananchi kuzithamini na Kuona umuhimu Wa kuitembelea hifadhi za Taifa 

Imekuwa ni kawaida kwa watanzania kuwashuhudia watalii kutoka nje ya nchi kuzitembelea hifadhi zetu za Taifa huku zikiwa karibu nasi. 

Kumekuwa na dhana kuwa Watanzania tunashindwa kutembelea mbuga hifadhi zetu kutokana na gharama zinazotozwa kama kiingilio.

Ni dhahiri kuwa ni asilimia ndogo ya Wananchi Wa Tanzania ambao tunayajua mengi kuhusu umuhimu Wa hifadhi zetu za Taifa. Walio wengi husikia kutoka kwa wachache waliowahi kwenda katika baadhi ya hifadhi zetu.

Wengi husikia taarifa za hifadhi zetu kutoka kwa wanafunzi ambao Mara kwa Mara wanapata fursa za ziara mbalimbali kuzitembelea hifadhi hizo ikiwa sehemu yao ya mafunzo.

Imekuwa jambo rahisi kwa mgeni anaetoka Ulaya , Amerika , au sehemu yeyote duniani  kuzitembelea hifadhi ambazo zipo karibu nasi na kuzijua zaidi hifadhi zetu kuliko sisi tuliokaribu zaidi.

Kuona umuhimu Wa kila Mwananchi kutembelea hifadhi na zetu na kuwa balozi mzuri Wa hifadhi zetu kwa wananchi wengine na hata wageni wanaokuja kuitembelea nchi yetu.

Sisi kuwa mabalozi Wa hifadhi zetu wenyewe itaongeza thamani ya mbuga zetu za wanyama , wanyama wetu adimu, na kila hifadhi zetu adimu ulimwenguni.

Hifadhi za Taifa TANAPA imetoa fursa umuhimu na ya pekee kuwahi kutokea nchini . 

Ofa hii ya siku tagu inatoa fursa kwa wananchi kutembelea hifadhi za Taifa bure yaani bila kiingilio kwa kipindi cha si Ku TATU kuanzia tarehe 2 hadi 4 June 2017. 

Hifadhi za Taifa TANAPA imeondo gharama za kiingilio katika kutembelea hifadhi zetu ndani ya siku hizo mbili.

Hapa chini nimekuwekea Taarifa ya hifadhi za Taifa TANAPA.




Endelea kubaki nami ikiwa ni pamoja na kwenye Mitandao ya kijamii Facebook ,Twitter, Instagram,  kote kwa jina la Habari Tanzania Grace Macha  bila kusahau kutazama Latest Videos zote katika V.O.A TV YouTube.

4 comments: