Friday, May 26, 2017

Updates: 1 Billion yahitajika kuwatibu watoto wahanga wa Ugonjwa wa Moyo


Waziri wa Maliasili na utalii Mh. Jumanne Maghembe akiagana Bw. Willey Chambulo M/Kiti TATO.

Billion I 1 yahitajika kwa ajili ya kutoa msaada wa kuwatibu watoto wanaokabiliwa na tatizo la moyo nchini.

Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Karibu Fair mwaka huu jijini Arusha M/ Kiti wa TATO amesema kauli mbiu ya maonesho ya Karibu Fair mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu ya 'MOYO MIAMOJA'  

Amesema kauli mbiu hiyo inakuja wakati ambapo nchi inakabiliwa na tatizo la ugonjwa wa moyo hususani watoto ambapo fedha kiasi cha millioni 30 imekuwa ikitumika kumtibu mtoto mmoja nchini India. 

Huku kwa hapa nyumbani matibabu hayo yakipatikana kwa gharama nafuu ya shilingi millioni 10 tu. " India mtoto mmoja anatibiwa kwa shilingi millioni 30 gharama ambayo in kubwa mno.." Mh. Chambulo

Zaidi ya fedha 1 bilion zinahitajika kusaidia kutibu watoto wanosumbuliwa na tatizo la moyo nchini " tunahitaji kiasi cha shilingi billioni 1 kuwatibu watoto mia tank (500) had I sasa imepatikana millioni 92), ikiwa ni michango toka kwa wadau mbalimbali wa sekta binafsi" Alisema Mh Chambulo

Maonesho ya Karibu fair mwaka huu yamefana jijini Arusha ikiwa kitovu cha utalii nchini ambapo yamehudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe.
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JUMANNE MAGHEMBE

Katika hotuba yake Mh. Maghembe Amesema no muhimu kuliweka soko la utalii hapa nyumbani ili iwe rahisi kutangaza utalii.


Katika hatua nyingine Waziri huyo amesisitiza kuwathibiti Majangili ambao ni tishio kwa mbuga zetu kwa kusababisha madhara na kuikosesha pato taifa.

No comments:

Post a Comment