PICHA: Baa la Njaa Kuikumba Somalia


Mtoto ambaye anaugua utapiamlo nchini Somalia.(Picha:IOM/Muse Mohammed)
Picha zenye kushtua na kujenga simanzi kuhusu janga la ukame katika maeneo sita kaskazini na magharibi ya kati mwa Somalia zimeonyeshwa leo mbele ya waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM. Flora Nducha na maelezo zaidi kuhusu picha hizo.
Sadir mwenye umri wa miaka miwili akimlilia mama yake Imran katika kitengo cha watoto mahututi, Kismayo, Somalia.Picha:IOM/Muse Mohammed
(Taarifa ya Flora)
Nats..
Maelezo hayo kutoka kwa mpiga picha wa IOM, Muse Mohammed ambaye amefanya ziara ya miezi sita katika maeneo mbalimbali nchini Somalia, akisema janga aliloliona ni halisi.
Picha zinaonyesha mizoga ya wanyama, mito iliyokauka, mtu akichimba ardhi kwa muda wa saa moja na nusu kusaka maji, msichana mwenye umri wa miaka 6 ambaye amepoteza baba na kaka yake kutokana na njaa, ikiwa tu ni baadhi ya athari hizo..
(Sauti ya Muse)
“Inashtua sana kuona watoto walioathirika chini ya umri wa miaka mitano, kwenda katika maeneo sita inaonyesha jinsi hali hii inavyoathiri maeneo mbalimbali, na kwa bahati mbaya pia nimeona watoto waliofariki, na huyu amefariki muda mchache tu nilipofika”.
Hakima, mwenye umri wa miaka mitano, akionyesha dalili za unafuu katika kitengo cha wagonjwa mahututi. Picha:IOM/Muse Mohammed
Ziara kama hiyo Somalia imefanywa pia na Marixie Mercado wa UNICEF ambaye amesema kwa alichoshuhudia..
(Sauti ya Marixie)
“Tunatarajia ongezeko la asilimia 50 ya idadi ya watoto wenye utapiamlo au watakaopata utapiamlo uliokithiri na hivyo kuwa milioni 1.4 mwaka huu. Hii itajumuisha watoto 275,000 ambao wana utapiamlo uliokithirii, watoto ambao wako mara tisa zaidi kufariki dunia kutokana na magonjwa kama kipindupindu, kuhara, na surua.”

0 Comments:

Post a Comment