MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAJITOKEZA KWENYE MAZIKO YA MEYA WA ZAMANI WA JIJI HILO.



Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam leo Alhamisi wamejitokeza kwa wingi katika maziko ya Mzee Kitwana Kondo ambaye alikuwa Meya wa zamani wa jiji, Mbunge wa zamani wa Kigamboni na mwanasiasa mkongwe ambae ameaga dunia jana.
Mwanasiasa mkongwe Kingunge Gombale

Katika mazishi hayo, walikuwemo viongozi wakuu wastaafu wakiongozwa na Rais Mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi, Waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa, Waziri wa zamani wa ulinzi Mh. Edgar Maokola Majogo, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Mzee Juma Mwapachu, Katibu mkuu wa CCM Mh. Abrahman Kinana na viongozi mbali mbali wa kidini.

Marehemu Kitwana Kondo ameugua na kuwa katika hali ya umahututi kwa zaidi ya miaka minne, mpaka umauti unamkuta alikuwa na umri wa miaka 92.

Mungu aiweke roho ya Marehemu Kitwana Kondo pema peponi, Amin.
PICHA ZOTE .: Mh.Edward Lowassa akiwakatika picha mbalimbali na viongozi pamoja na wananchi mbalimbali.

0 Comments:

Post a Comment