JAPAN: Group la pili la askari wa SDF ya Japan limerejea likitokea Sudan

Kundi la pili la askari wa SDF wa Japani warejea kutoka Sudan Kusini
Askari zaidi ya 100 wa Kikosi cha Kujihami cha Japani, SDF waliokuwa katika jukumu la kulinda amani Sudan Kusini chini ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa wamerejea nchini Japani.

Ndege binafsi iliyowabeba askari hao 115 iliwasili jana Jumamosi asubuhi katika uwanja wa ndege mkoani Aomori Kaskazini mwa Japani. 

Hilo ni kundi la pili kurejea kati ya makundi manne ya askari 350 wanaotakiwa kurejea nchini Japani. Machi mwaka huu serikali ya Japani iliamua kuwarejesha askari wake wanaohudumu katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini. 

Ushiriki wa Japani katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini nchini Sudan Kusini umedumu kwa miaka mitano. Kundi la 11 na la mwisho la wahandisi waliotumwa nchini Sudani Kusini walishiriki katika miradi ya ujenzi wa barabara na miundombinu mingine katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba na maeneo mengine ya jirani tangu Disemba 12 mwaka jana. 

Moja ya majukumu mapya waliyopewa Vikosi vya Kujihami vya Japani chini ya sheria mpya ya usalama wa taifa ni kutumia silaha wanapokwenda kushiriki katika vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na matukio mengine yanayohusisha kushambuliwa. 

Kundi la tatu linatarajiwa kurejea Mei 14 na kundi la nne na la mwisho litareja Mei 27 mwaka huu

0 Comments:

Post a Comment